Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na wadau
mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa
mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya
Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu,
Dkt.Joseph Chilongani akizungumza na viongozi, watalaam,wafugaji na
wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la
kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani humo
Baadhi ya viongozi na watalaam wa
Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa
uhifadhi wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika
kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika Pori la akiba
la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao
wilayani Meatu.
Meneja wa Pori la Akiba la Maswa,
Lusato Masinde akiwasilisha taarifa yake kwa viongozi na watalaam wa
Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau mbalimbali wa
uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa mifugo katika
Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Katibu wa Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanayamapori ya Makao, Robert Simon akiwasilisha taarifa yake kwa
viongozi na watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na
wadau mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la
kuondoa mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
Mhifadhi kutoka Ranchi ya MWIBA,
Julius Makaroti akiwasilisha taarifa ya ranchi hiyo kwa viongozi na
watalaam wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu,wafugaji na wadau
mbalimbali wa uhifadhi katika kikao maalum cha kujadili suala la kuondoa
mifugo katika Pori la akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya
Hifadhi ya Wanyamapori ya Makao wilayani Meatu.
……………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka ameitaka ...
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya
Meatu mkoani humo, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Dkt. Joseph
Chilongani kutekeleza kwa weledi, uadilifu na haki zoezi la kuondoa
mifugo kwenye maeneo ya hifadhi litakaloanza September 04, 2017.
Mtaka ametoa kauli hiyo mara
baada ya viongozi wa Serikali na Chama Mkoa na Wilaya, Wataalam,
wafugaji na wadau wa uhifadhi na Utalii kukutana na kujadili suala la
uondoaji mifugo katika Maeneo ya Hifadhi, yakiwemo ya Pori la Akiba la
Maswa, Ranchi ya MWIBA na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) Makao
wilayani Meatu.
“Mkafanye zoezi hili kwa
weledi mkubwa na haki, lisije likawa zoezi la kuwaonea watu, kufanya
utapeli kwa kujifanya mnachukua ng’ombe kwa ajili ya kutaifisha halafu
mkagawana; viongozi na wote mtakaohusika mkalisimamie kwa makini sana
suala hili” alisisitiza Mtaka
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe.Joseph
Chilongani amesema baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi,
wafugaji na wadau wa uhifadhi na utalii ametoa muda wa siku nne na
kufikia Septemba 04 mwaka huu, wafugaji wawe wametoa mifugo katika
maeneo ya hifadhi kwa hiari.
Dkt.Chilongani amebainisha
kuwa Viongozi wa Wilaya ya Meatu walikutana na wafugaji katika maeneo
yao na kuwatahadhalisha juu ya uingizwaji wa mifugo kwenye maeneo ya
hifadhi, ili kuwasaidia waepuke adhabu ya kifungo na mifugo yao
kutaifishwa kwa kuwa kuingiza mifugo hifadhini ni makosa kwa mujibu wa
sheria.
“Maandalizi yote yako tayari,
timu za kutekeleza zoezi hili zote zipo, nitoe muda wa siku hizi
zilizobaki ili kufikia Jumatatu ya tarehe 04 zoezi la kuondoa mifugo
kwenye Pori la Akiba la Maswa, Ranchi ya MWIBA na WMA ya Makao lianze,
tulishawapa wafugaji muda wa kutosha tulipokuwa tukipita kwenye vijiji
kuzungumza nao juu ya madhara ya kuingiza mifugo hifadhini” amesema.
Kwa upande wake Meneja wa Pori
la Akiba la Maswa Lasato Masinde amezitaja baadhi ya changamoto za
kuingiza mifugo katika maeneo ya Hifadhi kuwa ni ushindani wa malisho na
maji kati ya wanyamapori na wafugwao,ongezeko la ujangili, kuuwawa kwa
wanyamapori hasa walao nyama, magonjwa na mmonyoko wa udongo kutokana na
wafugaji kukata miti.
Aidha, Masinde amefafanua kuwa
suala la uingizwaji wa mifugo katika hifadhi linachangiwa pia na baadhi
ya viongozi wa vijiji wasiokuwa waadilifu ambao hupokea fedha kwa
wafugaji na kuwaruhusu kuingiza mifugo yao, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
Meatu kuwachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kujihusisha na
uhalifu huo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wafugaji kupima
maeneo yao wanayomiliki na kuyawekea miundombinu ya mifugo kama vile
visima vya maji na mabwawa, majosho na mashamba ya malisho ili waweze
kufuga kisasa na kuondokana na adha ya kuhangaika kutafuta maji na
malisho.
Katika kikao hicho wafugaji
kwa pamoja wamekubali kutoa mifugo katika maeneo ya hifadhi na
kukubaliana na ushauri wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wa kupima maeneo yao na
kuweka miundombinu, hivyo wameomba watalaam wa Ardhi na Mifugo waweze
kuwasaidia namna wanavyoweza kutumia maeneo yao kufuga kisasa.
No comments:
Post a Comment