Pages

Wednesday, August 30, 2017

Prof. Mbarawa Aipa Tano TBIII

1


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akifafanua jambo kwa Eng, Emmanuel Raphael Wansibho Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi wa Viwanja vya Ndege huku Meneja Ujenzi wa Kampuni BAM inayojenga uwanja huo ya Eng. Ray Blumrick (kulia), akifuatilia.
2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akiangalia ramani ya namna muonekano wa miundombinu ya jengo la tatu la abiria litakavyokuwa mara baada ya ujenzi wake kukamilika (kulia), ni mtaalaam wa ramani toka kampuni ya BAM ya Uholanzi inayojenga uwanja huo akifafanua.
3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (katikati), akipata maelezo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria unavyoendelea kutoka kwa Meneja Ujenzi wa Kampuni ya BAM inayojenga uwanja huo Eng. Ray Blumrick (kushoto), ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika baadae mwakani umefikia asilimia 64 ya ujenzi wake na utahudumia abiria milioni sita kwa mwaka.
4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa (katikati), akipata maelezo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria unavyoendelea kutoka kwa Meneja Ujenzi wa Kampuni ya BAM inayojenga uwanja huo Eng. Ray Blumrick (kushoto), ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika baadae mwakani umefikia asilimia 64 ya ujenzi wake na utahudumia abiria milioni sita kwa mwaka.
…………………………..

Na Neema Harrison, TUDARCO
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ambapo sasa utakamilika Oktoba 2018.

Mhe. Prof. Mbarawa aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya mradi huo ulianza 2013, na sasa kuridhishwa na hatua waliyofikia.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo, Prof. Waziri Prof. Mbarawa amesema kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 64, na hatua iliyobaki ni ujenzi wa wa mifumo ya ndani ya jengo.
“Sote tumekuwa mashahidi nimekuwa nuikitembelea mara kwa mara ujenzi wa jengo hili na ninaridhika kwa kasi ya ujenzi wake, ambapo sasa tumefikia kwenye hatua nzuri na vitu vilivyobaki sio vikubwa kama ilivyokuwa wakati wanaanza, hivyo ni matumaini yangu hadi Oktoba mwakani (2018) jengo lote litakuwa limekamilika na serikali kukabidhiwa,” amesema Mhe. Prof. Mbarawa.
Hatahivyo, Prof. Mbarawa amesema serikali inatarajia kupata watalii wengi na serikali itapata mapato kupitia kodi na tozo za abiria wanaosafiri kutumia kiwanja hiki, pia wapangaji wanaotoa huduma mbalimbali yakiwemo maduka na usafiri wa magari.
Amesema serikali itaendelea kutoa fedha za ujenzi wa jengo hilo linalosimamiwa na mkandarasi BAM International ya Uholanzi, ambapo pia likikamilika litatoa ajira kwa Watanzania wengi.
“BAM wamekuwa wakifanya kazi nzuri nawapongeza sana na tunatarajia hadi kukamilika tutapata mradi bora utakaoliingizia taifa faida kubwa kutokana na kodi na tozo mbalimbali,” amesema Prof. Mbarawa.
Amesema jengo hilo likikamilika linatarajia kuchukua abiria milioni sita (6) kwa mwaka, na kupunguza msongamo ulipo katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII)

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment