Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza John Mongella (katikati), akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi baada ya kuzindua Klabu ya
Biashara mjini Mwanza hivi karibuni. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC,
Dk. Kassim Hussein. NBC imezindua Klabu ya Biashara iliyopewa jina la
‘NBC B-Club’ katika miji ya Kahama na Mwanza kwa kuandaa semina kwa
wafanyabishara wajasiriamali. NBC B-Club itasaida huduma
zisizo za kifedha kupitia mafunzo maalumu kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali kuhusu mbinu za uendeshaji wa biashara na kuwajengea uwezo
katika kuziendesha kwa ufanisi hivyo kukuza biashara hizo.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akihutubia wakati sherehe za
uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara jijini Mwanza hivi karibuni. Wengine
kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein, Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, John Mongella, aliyekuwa mgeni rasmi na Mkurugenzi wa
Kitengo cha Wateja Binafsi, Filbert Mponzi.
Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, John Mongella akihutubia wakati wa semina ya wafanyabiashara
katika uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC mjini Mwanza. Wengine
kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na Mkurugenzi wa Kitengo cha
Wateja Binafsi, Filbert Mponzi.
Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, John Mongella (katikati), akizungumza na ujumbe wa viongozi wa
NBC waliofika ofisi kwake kumtembelea wakiongozwa na Dk. Kassim Hussein
(kulia kwake) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theoblad Sabi
(kushoto kwake). NBC ilizindua klabu za biashara katika miji ya Kahama
na Mwanza pamoja na kusherehekea miaka 50 tokea ilipoanzishwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya mika 50 ya benki hiyo mjini Mwanza.
Mjumbe wa Bodi
ya NBC, Dk. Kassim Hussein (mwenye tai nyekundu), Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji, Theobald Sabi na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha
pamoja na wateja na waalikwa wengine wakijipiga picha maarufu kama
‘selfie’ kama moja ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 50 ya NBC
jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment