Pages

Thursday, August 31, 2017

MAAFISA WA WIZARA YA USHIRIKIANO WA MAENDELEO YA UJERUMANI WATEMBELEA MAHAKAMA YA AFRIKA


Afisa
Mawasiliano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki za
Binadamu(AfCHPR)Sukhdev Chatbar(kulia)akiwaongoza wageni kutoka Wizara
ya ushirikiano wa  maendeleo ya Ujerumani kupitia taasisi zake GIZ na
AGA waliotembelea mahakama hiyo wamekua ni wadau wakubwa katika kusaidia
miradi mbalimbali ya mahakama hiyo.

Mkutubi
wa Maktaba ya mahakama  hiyo,Revina Moshi akizungumza na maafisa kutoka
shirika la maendeleo ya kimataifa ya Ujerumani(GIZ),kutoka kushoto ni
Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa
Afrika(AU) ofisi ya Addis Ababa,Ethiopia,Barbara Schaefer,Janina Hasse
kutoka  Berlin,Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs

Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs akiangalia sehemu ya machapisho kwenye maktaba ya AfCHPR.

Msajili
wa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert
Enno(kulia)akizungumza na ujumbe kutoka taasisi za Wizara ya maendeleo
ya Ujerumani waliotembelea mahakama hiyo.

Msajili wa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert Enno akimkabidhi zawadi
Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa Afrika(AU) ofisi ya Ethiopia,Barbara Schaefer.

No comments:

Post a Comment