( Picha na Jeshi la Polisi).
……………………………………………………………………………………..
Na Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Simon Sirro amewataka madereva na wamiliki wa mabasi ya abiria
yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja na wamiliki na madereva wa
mabasi madogo ya abiria maarufu kama daladala kuhakikisha wanayafanyia
ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara magari yao ili kupunguza ajali
zinazosababishwa na ubovu na uchakavu wa
magari.
IGP Sirro aliyasema hayo jana
wakati alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika Kituo Kikuu cha mabasi
yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja na kituo cha daladala cha Mbezi
Luisi kwa lengo la kuangalia hali ya usalama wa kituo hicho, kuona
namna ukaguzi wa mabasi ya abiria unavyofanyika kabla hayajaanza
pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za abiria.
“Nimefarijika kuona watendaji wa
kituo hiki pamoja na askari wangu wakifanya kazi vizuri kwa ushirikiano
mkubwa hali inayosaidia kupunguza kero mbalimbali kwa watumiaji wa kituo
hiki” alisema IGP Sirro
Aliongeza kuwa Ubungo ni salama
na itaendelea kuwa salama kwa sababu vibaka wamepungua na wale
wanaofanya utapeli katika kituo hicho waache mara moja na kutafuta kazi
nyingine kwa kuwa mwisho wa siku wataacha familia zao baada ya kukumbana
na mkono wa sheria.
Pia ameelekeza magari yote ya
abiria yabandikwe namba simu zote za makamanda wa mikoa wa Kikosi cha
Usalama Barabarani pamoja na Wakuu wa Polisi wa wilaya zote sehemu
ambazo itakuwa ni rahisi kuonekana na abiria ili iwe rahisi kwao kutoa
taarifa pindi wanapoona dereva anaendesha gari kwa kukiuka sheria na
kanuni za usalama barabarani.
Aliwataka wananchi kuendelae
kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za uhalifu na
wahalifu ikiwa ni pamoja kutii sheria bila shuruti na kutoa wito kwa
wamiliki wa magari, madereva pamoja na abiria kuwa wastaabu na
kuhakikisha wanaheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani kwa kuwa
kila mmoja anafahamu madhara ya ajali.
No comments:
Post a Comment