Pages

Monday, July 3, 2017

MAONESHO YA SABASABA 2017: WENGI WAMIMINIKA KWENYE BANDA LA TRA KULIPA KODI YA MAJENGO

 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
OFISI nyingi za Mamlaka ya Mapato nchini, (TRA), habari kubwa ni "kodi ya majengo", hii ndiyo habari ya mjini hata huku mitaani. Idadi kubwa ya watanzania wameamua kwa hiari yao na hata kumshangaza Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kujitokeza kwa wingi kulipa kodi" Katuka historia ya nchi hii haijapata kutokea kuona watanzania tena kwa hiari yao wenyewe, wakiwa kwenye misururu mirefu wakisubiri kulipa kodi, hili ni jambo zuri na nimefurahishwa pia na TRA kuongeza muda wa kulipa kodi hiyo" Alisema Rais Magufuli wakati akifungua rasmi maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam Julai 1, 2017.
Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuona mwitikio wa wananchi kuwa mkubwa sana katika ulipaji wa kodi hiyo ya majengo, iliondoa tarehe ya mwisho ya kulipa kodi  kutoka Juni 30, 2017 na kuongeza wiki mbili zaidi hadi Julai 15, 2017 na hivyo kutoa fursa kwa wananchi kulipa kodi hiyo. Katika viwanja vya maonesho ya 41 ya biashara yakimataifa ya Dar es Salaam.
 Wananchi wakiwa wkenye foleni wakisubiri kuhudumiwa kwenye banda la TRA, lililoko viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu "viwanja vya sabasaba" barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Julai 3, 2017
 Mwananchi huyu akihudumiwa na afisa kodi wa TRA, Bi.Witness Msaki(kulia)
 Afisa kodi wa TRA, Bi.Witness Msaki, akipitia kumbukumbu za mwananchi aliyefika kupatiwa huduma
 Afisa kodi wa TRA, Bi.Judith Lwaikondo, akizungumza na mwananchi
 Afisa kodi wa TRA, Bi.Salome Charles, (kushoto), akizungumza na wananchi waliofika banda la TRA ili kulipia kodi ya majengo leo Julai 3, 2017.
 Bi Levina Shirima, Afisa Kodi TRA, akiwa kazini
 Bi.Salome, (kushoto), akimsikiliza mwananchi
 Bi. Judith Lwaikondo, Afisa kodi TRA akimuhumia mwananchi
Afisa kodi wa TRA, Bw.Ananias Kimbi, (kushoto), akimuhudumia mwananchi

No comments:

Post a Comment