Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF, Bw. William Erio, (mwenye suti), akiungana na wafanyakazi wenzake
kuhudumia wananchi wakati wa maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa uya
Dar es Salaam leo Julai 2, 2017. Wananchi wengi waliotembelea banda
hilo wamefurahishwa na huduma zitolewazo na wafanyakazi wake kwa kwa
jinsi wanavyosikiliza na kutoa huduma kwa wanachama na wananchi wengine.
miongoni mwa maswali mengi yaliyoulizwa mara kwa mara ni kuhusu mpango
wa uchangiaji wa hiari ujulikanao kama "Wote Scheme), unaotoa fursa kwa
wajasiriamali wadogo kama mama lishe madereva wa bodaboda, wamachinga na
mtu yeyote anayefanya kazi halali ya kumuingizia kipato anavyoweza
kujiunga na mpango huo na hatimaye kupata faida mbalimbali ikiwemo bima
ya afya na mikopo kwa wajasiriamali wadogo,
Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
Meneja wa elimu kwa wanachama wa Mfuko
wa Pensheni wa PPF, Bw. Kwame Temu, (kushoto), akitoa maelezo kwa
mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko jengo la Wizara
ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kuinakofanyika
maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam leo Julai 2,
2017
Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
Wafanyakazi wa PPF, wakiwa makini katika kuwahudumia wananchi waliofika banda la Mfuko huo
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William
Erio, (kushoto), akizungumza jambo, wakati alipokutana na muigizaji
mkongwe hapa nchini, Mzee Jangala, (wapili kushoto), wakati akitembelea
bustani daraza ya Jeshi la Magereza, kwenye maonesho ya 41 ya biashara
ya kimataifa ya Dar es Salaam, leo Julai 2, 2017. Wengine pichani kutoka
kulia ni Bi. Yunge Saganda wa Jeshi la Magereza, Bi. Lulu Mengele,
Meneja Uhusiano wa PPF na Bi Jannet Ezekiel Afisa Uhusiani Mwandamizi wa
Mfuko huo
Mama Anna Mkapa, (kushoto), ambaye ni
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, (EOTF), na Mke wa Rais
Mstaafu, Benjamin Mkapa, akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa PPF,
Bw. William Erio, (wapili kushoto), Mama Mwantumu Mahiza, wakati
alipotembelea banda la EOTF linalowakusanya wajasiriamali mbalimbali
kuitoka nchini kote leo Julai 2, 2017
Mjasiriamali kutoka mkoani Kigoma,
Bi.Dporothy Timoth Takwe, (kushoto), akitoa maelezo ya ladha nzuri ya
dagaa wa ziwa Tanganyika, wakati mama Mkapa, Mkurugenzi Mkuu wa PPF na
mmoja wa viongozi wa televisehni ya Agape, (kulia), wakati
walipotembelea banda la mjasiriamali huyo lililoko jengo la EOTF
Mama Mkapa, Mkurugenzi Mkuu Erio, wakitazama bidhaa zilizofungwa vizuri na wajasiriamali wa Tanzania
Bw. Erio akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Magereza
No comments:
Post a Comment