Na Mwandushji Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ameawaonya baadhi ya Wanasiasa kuacha
mara moja tabia ya kuwatetea watu wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama
kwa tuhuma za kujihusisha na uhalifu.
Rais Magufuli ametoa onyo hilo
leo Jijini Dar es Salaam wakati akiweka jiwe la msingi la
mradi wa
uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam.
“Kuna mwanasiasa anazungumza kuwa
hawa watu wamekaa sana lokapu (mahabusu) waachiwe wakati hawa watu
wanahusika na mambo ya ajabu katika nchi.
Kuna watu wamekufa kule zaidi ya
35, maaskari zaidi ya 15 na wanaohusika ni pamoja na hao lakini mtu
anatoka anazungumza kwamba wamekaa mno. Unaweza ukaona ‘By implication’
kwamba huyu lazima anahusika kwa njia moja au nyingine”, alionya Rais.
Amewataka wanasiasa wa namna hiyo kujifunza kunyamaza wakati serikali inafanya kazi yake.
Aidha Rais Magufuli alieleza
kusikitishwa na mmoja wa wanasiasa ambaye kimsingi hajawahi kusimama
hata siku moja kulaani mauaji ya watu wasio na hatia yanayotokea lakini
kwa kutaka sifa za kisiasa alisisimama hadharani kutaka wahalifu
waachiwe.
Alisema hivi karibuni jeshi la
Polisi lilikamata sare 6000 za jeshi na wanaohisiwa kuhusika ni pamoja
na ambao tayari wanashikiliwa na vyombo vya dola lakini bado mtu
anaingiza siasa kwa kuwatetea wahalifu.
Rais Magufuli ambaye pia ni Amiri
Jeshi Mkuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini, amelitaka jeshi la
Polisi kumhoji kwa kina mwanasiasa yeyote anayetetea wahalifu kwani
anaweza kuwa nae anahusika.
“Nataka Polisi mfanye kazi zenu,
hawa wanaoropoka waisadie polisi kupeleleza. Msiogope cha sura au mwendo
wa mtu awe na mwendo wa spidi au pole pole atayaeleza vizuri atakapo
kuwa mle lokapu.
Ameeleza kuwa yeye kama Rais moja
ya majukumu yake ni kulinda usalama wa Watanzania na kuusimamia kwa
nguvu zote na kwamba maendeleo yaliyopo yanakuja kwa sababu nchi ni
slalama.
Amewaomba Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao kutanguliza uzalendo na kutetea maslahi ya nchi.
Hivi karibuni aliyekuwa Waziri
Mkuu wa Tanzania, Edward Lowasa ambaye alijiuzuru kutokana na kashfa ya
mradi wa kuzalisha umeme wa Richmond alihojiwa na Polisi kutokana na
matamshi yake ya kutaka watuhumiwa wa kesi ya ugaidi kuachiwa kwa sababu
wamekaa mahabusu kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment