Meneja wa Mawasiliano Tigo, Woinde Shisael akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa J’aza Ujazwe Ujaziwe zaidi’ jijini Dar Es Salaam leo |
Waandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa mkutano huo mapema leo.
………………………………………………………………….
Kampuni
inayoongoza maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania, leo Tarehe 30Juni
2017, imezindua promosheni mpya na ya kusisimua inayoitwa ‘JazaUjazwe
Ujaziwe zaidi’ambapo wateja watakuwa wanazawadiwa vifurushi vya muda
wamaongezi, data na ujumbe mfupi kila mwezi kwa mwaka moja mzima
wanapokuwa wanaongeza salio,iwe ni kwa njia ya vocha za kawaida, e-pin
au Tigopesa.
Washindi
wa zawadi watapatikana kwa droo ambazo zitachezeshwa kila siku na kila
wiki ambapo wateja wote wa Tigo watakuwa na nafasi ya kujishindia GB 30
za data, dakika 3,000 za muda wa maongezi wa kupiga mitandao yote,
meseji 3,000 au kujishindia Samsung S8 kwa muda wa mwaka mzima.
Kwa
mujibu waTigo, promosheni hii inakuja sokoni kama sehemu ya kampeni
inayoendelea ya ‘JazaUjazwe’ ambayo ni shukurani za Tigo kwa wateja wake
kwa uaminifu wao usio badilika kwa kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni
hizo,Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo William Mpinga amesema,
“Tigoinathamini mchango mkubwa usio badilika ambao wateja wetu wamekuwa
wakitupatia kwa miaka mingi. Hii ndio sababu inayotufanya tuamini kuwa
wana haki ya kushukuriwa kwa uaminifu wao. Kama kampuni tunafuraha kwa
mara nyingine kuwazawaidia wateja wetu kwa kuwawezesha kuendelea
kufurahia dunia yetu -Huduma zetu zaki pekee”
Mpinga
alibainisha kwamba promosheni mpya itaimarisha Tigo kuwa ndio kampuni
inayotoa bidhaa na huduma zenye bei nafuu, wakati huohuo itakuwa
inaimarisha jukumu lake kama kampuni ya mawasiliano yenye ubunifu zaidi
Tanzania.
“Promosheni
hii imekuja kufuatia uboreshaji wa miundombinu ya mtandao wetu
uliofanyika hivi karibuni ambao unahakikisha utendaji wa hali ya juu wa
utoaji wa huduma. Kwetu sisiTigo, kila wakati tunakuwa wabunifu katika
kutengeneza mbinu mpya za kusisimua ambazo zinazo imarisha uhusiano wetu
na wateja wetu. Promosheni hii ya uaminifu ni njia bora ya kuwazawadia
na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma na bidhaa zetu.”
AlisemaMpinga.
Alithibitisha
tena kwamba Tigo imekusudia kuendelea kuwazawadia wateja wake kwa
bidhaa na huduma za kusisimua zaidi na akaongeza kwamba“Ubunifu wa
huduma na bidhaa zetu unatokanana utafitiwa kina unaolenga kuwaridhisha
wateja wetu. Kwa hiyo JazaUjazwe, Ujaziwe zaidi inakuja kukabiliana na
mahitaji ya wateja ya kuwa
na hisia ya msisimko kila mara wanapotumia huduma zetu. Tunaamini
kwamba wateja wetu watafurahia dakika, SMS au data za ziada wanazo
zawadiwa kila mara wanapoongeza salio na hivyo itaboresha mwenendo wa
mawasiliano yao” alielezea Mpinga
No comments:
Post a Comment