Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, akifungua kikao hicho, pembeni kulia ni Mratibu wa LVEMP Bw. Omari Myanza.
Baadhi ya Viongozi wa dini kutoka mkoa wa kagera wakiwa katika Warsha hiyo.
Baba
Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo katoliki Musoma Mkoani Mara
akiongea na Waandishi wa habari nje ya Mkutano huo kuelezea umuhimu wa
mazingira.
Sheik
Hassan Kabeke, akiafafnua jambo kwa waandishi wa habari nje ya Warsha
hiyo namna suala la mazingira linavyo tajwa katika Kuran tukufu.
Sheik
Hassan Kabeke, akiafafnua jambo kwa waandishi wa habari nje ya Warsha
hiyo namna suala la mazingira linavyo tajwa katika Kuran tukufu.
Mratibu
wa LVEM Akitoa maelezo ya awali kabla yakuanza kwa Warsha hiyo
ilikutanisha Viongozi wa Serikali na Dini katika baadhi ya Mikoa ya
kanda ya ziwa (Picha zote na Ofisi ya mkuu wa Mkoa Mwanza).
…………………………
Na Atley Kuni- Mwanza.
Serikali mkoani hapa, imewapa
jukumu kubwa viongozi wa dini kutoka baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa
kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega katika kulitunza ziwa Viktoria na
Maliasili zake ili liweze kuwa tegemeo kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Akifungua Semina ya siku moja
mkoani hapa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, na risala yake kusomwa
na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, Mongella amesema,
viongozi wa dini wanalo jukumu kubwa kwani wao husimamia imani za watu.
“Ninyi Viongozi wa dini dhima mliyonayo ndani ya jamii ni kubwa sana na
chochote mtakacho waelekeza waumini wenu lazima waweze kukitekeleza,
hivyo niwaombe sana viongozi wangu tulilinde ziwa viktoria kwa jitihada
zetu zote’’ alisema Mongella.
Aidha Mongella amesema kuwa, kuwepo kwa Ziwa Victoria ni fursa ya uendelezaji ya kauli mbiu ya “Tanzania ya Viwanda”
ambayo Serikali ya awamu ya Tano inasisitiza, “Ziwa hili linasaidia
upatikanaji wa rasilimali zinazotumika kwa matumizi ya nyumbani na
viwandani, usafiri na usafirishaji na uzalishaji wa nishati ya umeme
Hivyo basi hatuna budi kuhifadhi mazingira ya Ziwa na Bonde lake”
amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Kwa upande wao, viongozi wa dini
wakiongea wamesema, wao wanatambua na hata vitabu vya dini vinaelekeza
juu ya mwanadamu anachopaswa kufanya katika kulinda mazingira ikiwepo
ziwa Viktoria.
Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya
amani ya madhehebu ya dini katika Mkoa wa Mwanza, Sheik Hassan Kabeke,
amesema katika Uislam na hususan ni katika mafundisho ya Mtume Muhama
S.A.W, inafafanua juu ya mito miwili yaani mto Nile na Furabu ambayo
mtume aliipitia huku akisema kwamba, Mto Nile ambao unafungamanishwa na
Ziwa Viktoria Mtume amesisitiza kuyatunza mazingira, “Katika kupanda
miti kwenye uislamu mtu hupata thawabu, tunaimani kabisa kwamba kila
mmoja wetu akitunza mazingira ni sehemu ya Ibada, amesema Kabeke.
Naye Baba Askofu Michael
Msonganzila wa Jimbo Katoliki la Musoma, kwa upande wake amesema kwa
habari ya mazingira, tunaona ni jukumu la jamii nzima bila kujali
itikadi zetu “ Kukutana kwetu hapa tunataka kuangalia nikwa namna gani
tutaziangazia sababu za kiuchumi na kijamii, alisema Msonganzila na
kuongeza kwamba kwa sasa wao katika Mkoa wa Mara wanayo kampeni kwenye
eneo la Serengeti ambayo wanaendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa
Utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya hali ya nchi.
Mradi wa Hifadhi ya Mazingira wa
Ziwa Victoria (LVEMP II) utakamilika mwezi Disemba, 2017, aidha warsha
hiyo ni kati ya warsha nne zilizoandaliwa na Mradi kwa madhumuni ya
kukusanya maoni ya wadau ambayo yatawezesha kuandaa awamu ijayo ya Mradi
inayotarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2018.
Kikao hicho kimewakutanisha Wakuu
wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Viongozi wa dini kutoka
mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu na Mara.
No comments:
Post a Comment