Menejimenti
ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF inapenda kuwafahamisha
Wanachama na Umma kwa ujumla kuwa Ofisi ya Kanda ya Dar es Salaam iliyopo Mtaa
wa Mkwepu, Jengo la Diplomatic House,
katikati ya jiji la Dar es Salaam itahamia rasmi kwenye jengo la LAPF Millenium Towers, ghorofa ya tatu,
lililopo barabara ya Ali Hassan mwinyi eneo la Makumbusho kuanzia tarehe 01/07/2017. Hivyo wanachama na wadau
wote wa Mfuko wataendelea kupata huduma kulingana na matarajio yao katika
mazingira yaliyoboreshwa zaidi. Karibuni sana tuwahudumie.
“Ishi na Staafu kwa Ufahari
na LAPF”
No comments:
Post a Comment