NA
NATHANIEL LIMU- SINGIDA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto imetoa gari la
kubebeba wagonjwa kwa kituo cha afya cha Ndago kilichopo Wilayani Iramba mkoani
Singida.
Akikabidhi gari hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mh. Mwigulu Nchemba amesema Gari hilo litakuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa
eneo hilo kutokana na adha ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi wa kituo
hicho
Aliipongeza
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ambayo iliahidi kutatua
changamoto ya kero ya vifo vya wajawazito ambavyo vilikuwa vikitokea kutokana
na eneo hilo kukosa gari la wagonjwa.
“Kutokana
na huduma hafifu ya rufaa kwa wajawazito kwa kukosa magari ya wagonjwa, ukosefu
wa damu salama na ushiriki mdogo wa jamii katika mambo yanayohusu afya ya mama,
ikiwemo kuokoa vifo vitokanavyo na uzazi, serikali imeona umuhimu wa kutupatia
gari hili,” alisema mbunge huyo.
Aidha,
aliongeza kuwa nia yake kubwa mbali na kupata msaada huo wa gari la wagonjwa
pia atahakikisha anaboresha sekta ya afya katika jimbo, zahanati na vituo vyote
vya afya ili kuwapa fursa wananchi wapate huduma ambayo inastahili pamoja na
matibabu.
Pia
alisema anapambana vilivyo kuhakikisha kunakuwepo na vifaa vya tiba katika
maeneo husika pamoja na kuongeza idadi ya wauguzi, kwani anatambua bado kuna
changamoto nyingi katika sekta ya afya hivyo atajitahidi kadiri ya uwezo wake
ili kuongeza kasi ya kuboresha huduma hiyo ya afya.
Awali mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Ndago, Dkt Lyoce
Mgelwa alisema kipindi cha nyuma wagonjwa
walikuwa wanapata shida kubwa ya usafiri na wakati mwingine walishindwa kwenda
kupatiwa matibabu kwa muda muafaka na kusisitiza kuwa hakuna mwananchi yeyote
atakayetozwa gharama katika kutumia gari hilo.
Kwa upande wake Jumanne Hatibu mkazi wa kijiji cha Urughu tarafa
ya Ndago alisema kabla ya ujio wa ambulance hiyo kijiji hicho kilikuwa kinakabiliwa
na tatizo sugu la usafiri kwa wagonjwa hasa akina mama wajawazito.
Waziri
wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Mkoani Singida Mwigulu Nchemba
akiwasha gari la kubebea wagonjwa (ambulance), katika kijiji cha Urughu tarafa
ya Ndago jimbo la Iramba.
Mkazi
wa kijiji cha Urughu jimbo la Iramba mkoani Singida Jumanne Hatibu akizungumza
kwenye hafla ya makabidhiano ya gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na
serikali kupitia wizara ya afya jinsia, wazee na watoto
No comments:
Post a Comment