Prof. Ninatubu Lema, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania, (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame
Mbarawa (wa tatu kutoka kulia), leo wakati akianza ziara ya kutembelea
jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA_TBIII).
Meneja
wa Mradi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Ray Blumrick (kushoto) akitoa
ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye ujenzi wa jengo hilo, ambapo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbarawa (wa tatu
kutoka kushoto) akimsikiliza kwa makini.
Mhandisi
Simba Charles (aliyenyoosha mkono) akionesha eneo la maegesho ya magari
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa
(katikati), leo alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa jengo la tatu
la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Bw. Ray Blumrick, Meneja Mradi wa
jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA-TBIII) akimwelekeza namna paa lilivyo imara, Prof. Makame
Mbarawa (Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano) aliyetazama juu
katikati wakati wa ziara yake kwenye jengo hilo leo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Prof Ninatubu Lema akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa pili kutoka
kushoto) leo alipofanya ziara ya kutembelea jengo la tatu la abiria la
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Kulia ni Mkurugenzi
wa Fedha wa TAA, Bw. Richard Malulu.
No comments:
Post a Comment