Mabingwa wa Afrika Zambia wametokea
nyuma na kuifunga Ujerumani kwa magoli 4-3 katika muda wa ziada na
kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia U20 Korea Kusini.
Zambia ilionekana kama imeshinda
mechi hiyo ikiwa inaongoza kwa magoli 3-1 katika dakika ya 89, lakini
magoli ya Suat Serdar na Jonas Arweiler yalifanya ngoma kuwa sare.
Katika mchezo huo shujaa alikuwa ni
Shemmy Mayembe kwa kuifungia Zambia goli la mapema katika kipindi cha
pili cha dakika 30 za ziada.
Kwa matokeo hayo Zambia sasa
watavaana na Ufaransa ama Italia katika hatua ya nane bora siku ya
jumatatu.
No comments:
Post a Comment