Pages

Wednesday, May 3, 2017

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PROF. PALAMAGAMBA KABUDI AHUDHURIA MKUTANO WA 56 A MWAKA WA JUMUIYA YA MASHAURIANO YA MASUALA YA KISHERIA YA NCHI ZA ASIA NA AFRIKA

Q 2
Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ya kisheria yanayohusu ugaidi, utawala wa sheria, maendeleo ya Mahakama ya Kimataifa ya mauala ya Jinai na masuala ya wakimbizi katika nchi wanachama.
AALCO ilianzishwa mwaka 1956 kwa lengo la kuwa chombo cha ushauri na ushirikiano katika masuala ya sheria za kimataifa kwa nchi za Asia na Afrika. Toka kuanzishwa kwake chombo hiki kimewezesha nchi wanachama kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya sheria za kimataifa na kimechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sheria za kimataifa.
Tanzania ilijiungana umoja huo 1973 na kwa sasa Katibu Mkuu wa Umoja huo ni Mtanzania Prof. Kennedy Gastorn ambaye alichaguliwa kushika nafasi hiyo Agosti 2016.

No comments:

Post a Comment