Waziri wa Viwanda,Biashara
naUwekezaji Mhe. Charles Mwijage kulia akipokea cheti cha chanjo cha
kimataifa kijulikanacho kama cheti cha homa ya manjano kutoka kwa Afisa
Afya Bw. Fadhili Kilamile mara baada ya kupata chanjo hiyo leo kwenye
viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe.
Mussa Zungu wa kwanza kulia akisubiria kupewa cheti cha chanjo cha
kimataifa kijulikanacho kama cheti cha homa ya manjano kutoka kwa Kaimu
Mkuu wa Kitengocha Afya Mipakani Bw. Remidius Kakulu kushoto mara baada
ya kupata chanjo hiyo leo kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
MbungewaVitiMaalumjimbo la
SingidaMhe. Martha Mlatawa kwanza kuliaakiandikiwacheti cha chanjo cha
kimataifakijulikanachokamacheti cha homayamanjanokutokakwa Afisa Afya
Agnes Shirima
katikatimarabaadayakupatachanjohiyoleokwenyeviwanjavyabungemjini Dodoma
aliyesimamani Afisa Habari wa WizarayaAfya Bi. Catherine Sungura.
…………………………
Na.Catherine Sungura, WAMJW
Dodoma
Watanzania hususan wale
wanaosafiri nje ya nchi zile zenye ugonjwa wa homa ya manjano wanatakiwa
kujitokeza kwenye vituo vilivyoainishwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa ajili ya kupata chanjo hiyo pamoja na
kubadilisha vyeti mpya
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati alipofika
kupata huduma ya chanjo ya homa ya manjano ambayo inatolewa bungeni hapa
Waziri Mwijage amesema duniani
ugonjwa huu upo na zipo nchi nyingi ambazo zimepoteza wananchi wake kwa
kuugua ugonjwa huo“Suala hili ni muhimu sana kwa afya zetu,pamoja na
kwamba nchi yetu haina mgonjwa wa homa ya manjano
Aidha amesema maambukizi ya
ugonjwa huu endapo mtu ataupata gharama za matibabu yake ni ghali sana
na inaweza kupelekea kupoteza maisha,hivyo ni vyema kujitokeza kwa wingi
kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha kadi zao kwani usiweke reheni
maisha yako
Hata hivyo aliwatahadharisha
wafanyabiashara,wanafunzi wale wanaosafiri au kusoma nje ya nchi ni
vyema wahakikishe wanapata chanjo hiyo kuliko kupewa kadi kwa njia
nyingine kwani kadi hizi zimeboreshwa na zina alama za siri ambazo nchi
za kimataifa zina uwezo wa kusoma alama zetu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ilala
Mhe.Mussa Zungu ameipongeza Wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia
Wazee na Watoto kwa kubadilisha kadi hizi mpya kwa kuepukana na vyeti
vingi ambavyo vilikua vinanunuliwa mtaani bila kupata huduma za kupata
chanjo,hivyo ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanapata chanjo hizo
kwani ilikua ni hatari sana hususan nchi zile zenye milipuko wa homa za
manjano na hivyo kupata vyeti ambavyo ni halali
Wizara ya Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto limeongeza muda wa kubadilisha vyeti vya
zamani hadi mwisho wa mwezi huu na baada ya hapo vyeti vya zamani
havitatambulika tena.
No comments:
Post a Comment