Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiwasisitiza wakazi
Lamadi mkoani Simiyu umuhimu wa kumiliki ardhi kwa hati kwa kuwaonesha
moja ya hati zinazotolewa kwa wananchi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akikagua moja ya faili
katika masijala ya Ardhi ya Ilemela Mkoani Mwanza akiwa na Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza John Mongela (mwenye kofia).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiongea na wakazi wa Ilemela mkoani Mwanza.
Magere Mugeta mkazi wa Lamadi
mkoani Simiyu akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Janet Magige mkazi wa Lamadi
mkoani Simiyu akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Baadhi ya wakazi wa Ilemela
mkoani Mwanza wakiimba nyimbo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi alipokuja kusikiliza kero
zao za ardhi katika eneo lao.
……………………………………………………..
Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi amegawa hati miliki za ardhi
122 kwa wananchi wa Lamadi Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara yake
mikoa ya kanda ya ziwa kuhamasisha ulipaji kodi ya pango la ardhi na
suala la urasimishaji wa
makazi holela.
Wananchi hao 122 ni
wale waliofanikiwa kulipia michango yote, hivyo kuondokana na makazi
holela na kuishi katika makazi rasmi. Hata hivyo jumla ya wananchi 5,200
wa Lamadi Mkoa wa Simiyu washapimiwa maeneo yao kwa ajili ya
urasimishaji, na watapatiwa hati zao mara tu baada ya kukamilisha
michango stahili.
Katika ziara hiyo,
waziri Lukuvi amefika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza na kufanya ukaguzi
wa mfumo wa ulipaji kodi ya pango la ardhi wilayani hapo na kugundua
kati ya wakazi 35,000 wanaotakiwa kulipa kodi ya ardhi 28,000
wameishapelekewa hati ya madai.
Waziri Lukuvi pia
ametembelea Idara ya Ardhi ya wilayani Nyamagana na kukagua mafaili ya
kumbukumbu za wananchi kuhusu taarifa za ardhi ikiwemo masuala ya hati
na kukugundua baadhi ya viongozi hawajalipa kodi ya pango la ardhi.
Mmoja ya viongozi hao ni Mbunge wa Kwimba Shannif Mansoor ambaye
hajalipa kodi ya pango la ardhi tangu 2010 kiasi cha shilingi milioni
529.
Aidha katika wilaya
hiyo ameongea na wananchi wa Nundu kata ya Meko, mbali ya kusikiliza
kero zao na kuzipatia ufumbuzi papo hapo, amewahimiza kuchamkia fursa
ya kurasimisha makazi yao na kupata hati ili kuzipa thamani ardhi zao na
kujitanulia fursa za uchumi.
No comments:
Post a Comment