Ofisa Programu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Alphonce Slima, akiongoza semina ya kujadili vipaumbele katika bajeti ya Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha
wa 2017/2018 iliyofanyika makao makuu ya TGNP Mabibo jijini Dar es
Salaam jana.
Mdau Neofita Kunambi akizungumza wakati akichangia mada kwenye semina hiyo.
Anna Sangai akichangia jambo kwenye semina hiyo.
Sadick
Juma mkazi wa Mbezi Beach, akielezea changamoto ya upatikanaji wa dawa
na vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili.
Janeth Mawinza akielezea changamoto ya matibabu ya homa ya ini ambayo dawa zake hazipatikani nchini hadi zitoke India.
Moses
Benard akizungumzia wajawazito kujinunulia vifaa vya kujifungulia na
suala la dawati la ukatili wa kijinsia kuwepo vituo vya polisi.
Mdau Dalia Kalungwana akichangia jambo.
Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
wananchi wakifuatilia kwa karibu semina hiyo.
Vijana wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI
wameiptia bajeti ya mwaka 2017/ 2018 ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto iliyotengwa na kuomba iongezwe kwa
kuzingatia ukubwa wa wizara hiyo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao
wa Kijinsia Tanzania (TGNP) ya majadiliano ya kupitia bajeti hiyo ili
kuona vipau mbele vyake waliombwa iongezwe ili iweze kukabiliana na
changamoto zilizopo kwenye wizara hiyo ambayo imelemewa kutokana na
ukubwa wake.
Kwa mwaka
wa fedha wa 2016/ 2017 wizara hiyo ilitengewa bajeti ya sh.bilioni 845
ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2017/2018 ambayo tofauti yake sio
kubwa.
Akizungumza
katika semina hiyo, Neofita Kunambi alisema katika wizara hiyo
kunachangamoto kubwa bila ya kuongezewa fedha katika bajeti yake
hazitaweza kuisha.
“Bila ya
kuongeza bajeti katika wizara hii wajawazito wataendelea kujinunulia
vifaa vya kujifungulia tunaomba jambo liangaliwe kwa karibu” alisema
Kunambi.
Anna
Sangai alisema huduma za afya zinapaswa kuboreshwa kuanzia upatikanaji
wa dawa na vifaa tiba na bila kuongezwa kwa bajeti katika wizara hiyo
itakuwa ni ndoto.
Mkazi wa
Mbezi Beach, Sadick Juma alisema upatikanaji wa dawa, vifaa tiba,
miundombinu na ukatili wa kijinsia ni changamoto kubwa katika wizara
hiyo.
Alisema
licha ya kuwepo duka la Bohari ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya Rufaa
ya Taifa ya Muhimbili (MNH), upatikanaji wa dawa umekuwa mgumu hivyo
kuifanya Muhimbili kuwa na majengo mazuri bila ya kuwa na dawa.
“Ukitaka
kuona changamoto hata ukiwa ni mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya
afya (NHIF) ugua au uwe na mgonjwa ambaye ni mwanachama uende katika
hospitali hiyo kwanza kupokelewa tu pale mapokezi ni balaa na ukifika
muda wa kutakiwa kupata dawa utaambulia panado na kuambiwa dawa hazipo”
alisema Juma.
Juma
aliongeza kuwa huduma ya bure kwa watu wenye msamaha hiyo ni ndoto kwani
wagonjwa hao hawasikilizwi kabisa jambo ambalo ni hatari.
Alisema
serikali imekuwa ikijipodoa kuwa inaboresha huduma za afya lakini hali
halisi haipo hivyo akitolea mfano kwa nchi nzima maduka ya dawa ya MSD
yapo nane tu je upatikanaji wa dawa na vifaa tiba utafikia katika
kiwango cha kukidhi mahitaji alihoji Juma.
Janeth
Mawinza alisema bajeti hiyo iangalie zaidi jinsi ya kutibu magonjwa kama
ya homa ya ini ambayo matibabu yake kwa hapa nchini hayapatikani mpaka
dawa itoke nchini India.
Moses
Benard alisema ikiwa mjamzito aliopo mjini anatakiwa kujinunulia vifaa
vya kujifungulia hali ikoje kwa yule ambaye yupo kijijjini ambaye
anachangamoto ya kutokuwa na fedha na kukimbiwa na mwenza wake hivyo
akaomba Waziri wa wizara hiyo kutoa tamko rasmi la kuwataka wajawazito
kutonunua vifaa hivyo wanapokwenda hospitali kujifungua.
Wadau
wengine waliongelea jijini Dar es Salaam maeneo mengine kama Kipunguni
wilayani Ilala kukosa kuwa na zahanati au hospitali hivyo kulazimika
kwenda wilaya ya Kisarawe kupata matibabu jambo ambali linashangaza
hivyo wakaomba bajeti ya wizara hiyo iongezwe ili kufanikisha
upatikanaji wa zahanati au hospitali katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment