Pages

Wednesday, May 3, 2017

CRISTIANO RONALDO AFUNGA HAT-TRICK YAKE YA PILI KATIKA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Mchezaji nyota duniani Cristiano Ronaldo amefunga hat-trick yake nyingine katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Real Madrid ikiichakaza Atletico Madrid kwa magoli 3-0 katika mchezo wao wa kwanza wa nusu fainali.

Real Madrid waliutawala mchezo huo na kuwadhibiti mahasimu wao hao wa kuu wa mji mmoja katika dimba la Bernabeu na kuongoza katika dakika ya 10 tu baada ya Ronaldo kufunga goli la kwanza kufuatia krosi ya Casemiro.

Ilionekana kama wenyeji Real Madrid wanaweza kushindwa kutumia vyema dimba la nyumbani hadi pale Ronaldo tena alipofunga goli la pili kwa shuti kali na kisha baadaye kupata goli rahisi la tatu kupitia pasi ya Lucas Vazquez.
                Cristiano Ronaldo akiruka juu na kufunga kwa mpira wa kichwa goli la kwanza
          Kiungo Toni Kroos akimdhibiti mshambuliaji nyota wa Atletico Madrid Antoine Griezmann
3FDFD18400000578-4467182-image-m-62_1493756654097
Hattrick yake ya 7 katika michuano ya Champions League imemfanya Cristiano Ronaldo aifikie rekodi aliyokuwa nayo Lioneil Messi katika mashindano hayo ya UEFA.
Cristiano Ronaldo alikuwa mwiba mchungu kwa Atletico Madrid kwani mabao matatu aliyofunga, moja kipindi cha kwanza na mawili kipindi cha pili yalitosha kuiangamiza kabisa
Atletico Madrid.
Real Madrid wanaendeleza ubabe wao kwa Atletico Madrid katika michuano ya Champions League kwani toka mwaka 1958 Atletico Madrid hawajawahi kuitoa Real katika mchuano hiyo.
Matokeo hayo yanaiweka Real Madrid katika nafasi kubwa kucheza fainali ya Champions League msimu huu kwani mechi ya pili itawabidi Atletico kuwafunga Real mabao manne ili wafudhu.
Katika mchezo huo Atletico Madrid walionekana kupwaya sana kwani hadi kipindi cha kwanza kinaisha walikuwa hawajapiga hata shuti moja kuelekea langoni kwa Real Madrid.
Atletico watawakaribisha Real wiki ijayo kujaribu kubadili matokeo haya ya mwanzo, leo inapigwa nusu fainali ya pili ambapo Monaco wataikaribisha Juventus.

No comments:

Post a Comment