Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amehitimisha kilele cha Maadhimisho
ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika kitaifa
Jijini Mwanza.
Mongella
amewasisitizia wanahabari kujikita zaidi katika weledi kwenye utendaji
wao wa kazi ili kuondokana na migogoro inayoweza kujitokeza wakati
wakitimiza majukumu yao.
Amewahimiza
zaidi waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi na
utafiti wa kina katika habazi zao huku akihimiza zaidi ushirikiano.
#BMGHabari
Kamanda
wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) akifuatilia maadhimisho
hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa
Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari.
Rais
wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deogratius
Sonkolo (kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini TEF, Theophil
Makunga (kushoto), wakifuatilia maadhimisho hayo.
Mkurugenzi
wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Abubakar Karsan,
akichangia mada kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani, kitaifa Jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment