Meya wa jiji la Dar es SAlaam
Isaya Mwita akimfariji Mjane wa aliyekuwa mhasisi na Katibu MKuu wa
kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bob Makani( Mama
Makani)
Mjane wa aliyekuwa mhasisi na Katibu MKuu wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema Kaboga Makani akimueleza jambo Mstahiki
Meya wa jiji la Dar es SAlaam Isaya Mwita mara baada ya kumtembelea
Nyumbani kwake mapema leo asubuhi.picha zote na Christina Mwagala, OMJ.
Meya wa jiji amtembelea Mjane wa Bob Makani nyumbani leo
NA CHRISTINA MWAGALA, OMJ
MEYA
wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amemtembele mjane wa aliyekuwa
Mhasisi na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Bob Makani , Mama Kaboga Makani ikiwa ni moja ya ziara zake za
kutembelea wazee pamoja na viongozi ambao waliwahi kushika nafasi
mbalimbali za uongozi ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Meya
ambaye amerejea Nchini jana kutoka Nchini Iran ambapo alikuwa kwa ziara
ya kikazi ya siku 10, amesema kwamba hatua ya kutembelea viongozi
pamoja na wazee ambao ni waasisi inalenga kutambua michango yao katika
nafasi ambazo waliwahi kutumikia na kwamba busara zao pia ndio zimeweza
kulifikia Taifa sehemu ilipo hivi sasa.
Alifafanua
kuwa Bob Makani enzi za uhai wake alikuwa ni mmoja na mwa sisi wa
Chadema na kwamba anatambua mchango wake kutokana na juhudi
alizozionyesha ikiwemo kukipigania chama hadi kufikia kilipo hivi sasa.
Alisema
Bob Makani pamoja na wenzake ndio waliokianzisha Chama Cha Chadema na
kufika mbali zaidi kwamba bila wao hata yeye asingekuwa Meya wajiji hili
kupitia chama hicho na kwamba mchango wao ndani ya chama bado
utaendelea kukumbukwa na kila mmoja wakiwemo wanachama wa chama hicho na
wananchi kwa ujumla.
Alisema
Bob Makani mbali na kuwa mwanachama na mwasisi wa Chadema lakini pia
aliwahi kuwa Gavana wa Benki kuu ambapo alitumikia nafasi hiyo kwa na
hivyo baada ya kustaafu nafasi hiyo aliamua kuanzisha chama na hivyo
kuwepo hadi hivi sasa.
“ Haya
sio mambo ya kisaisa , lakini unaweza kuona kwamba ni alikuwa mtu
muhimu , lakini pia kama kijana wao lazima nipate basara kutoka kwao,
ingawaje hatunaye tena hapa duniani, lakini huko alipo anaona jambo gani
ambalo tunafanya kama vijana ambao alituacha ndani ya chama” alisema.
Alifafanua
kwamba jambo la kutembelea viongozi ama waasisi wa nafasi chama sio
jambo la kisiasa bali ni kutokana na kutambua mchango wakazi ambazo
waliwahi kuzifanya wakati huo.
“ Ziara
hii sio ya kwa Mzee Makani tu, ila ni kwa waasisi , na wale ambao
waliwahi kuwa viongozi wa jiji, wapo nitawatembelea, ikiwa ni sehemu
yangu pia ya kutambua mchango wao, sambamba na kupata baraka , busara
zao ambazo walizitumia katika uongozi wao, ukizungumza vizuri na wazee
hawa unapata baraka na kuona kwamba namna gani unaweza kuwaongoza
wananchi” alisema Meya Mwita.
“ Nimekuja
leo kumuona Mama yetu, naweza kusema ni mama yetu kwa sababu kila mmoja
anamfahamu mzee Makani , alikipigania chama, na ndio katibu mkuu wa wa
kwanza ndani ya Chadema, kama vijana hatuna sababu ya kuwasahau wasisi
wetu, wazee wetu, watu ambao tunawatambua kabisa waliitumikia nchi yetu”
alisema Meya Isaya.
No comments:
Post a Comment