Mkurugenzi
wa Utumishi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makwaia Makani
ambaye anamwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru
– kizungumza na madaktari kutoka Hospitali ya BLK ya India wanaohusika
na upandikizaji wa figo na wataalamu wengine.
Kutoka
kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa mfumo wa Mkojo, Dk Hardev
Bhatyal wa Hospitali ya BLK ya nchini India, Mkuu wa Maabara wa BLK, Dk.
Anil Handoo na Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo, Vigyat Singh
wakimsikiliza mkurugenzi wa Utumishi, Makwaia Makani leo.
Mkurugenzi
wa Huduma za Upasuaji, Dk Julieth Magandi wa Muhimbili, Mkurugenzi wa
Huduma za Tiba Shirikishi wa MNH, Dk Praxeda Ogweyo, Mkurugenzi wa
Uuguzi, Agnes Mtawa wa MNH na Mkuu wa Idara ya Urolojia wa hospitali
hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro wakifuatilia mkutano huo leo.
Madaktari na wataalamu wengine wa Hospitali ya BLK kutoka India wakitembelea vyumba vya upasuaji Muhimbili leo.
Madaktari
na wataalamu wengine wa Hospitali ya BLK kutoka India na wenzao wa
Muhimbili wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare
(kushoto) wakati walipotembelea idara hiyo leo.
Wageni hao wakiwa katika chumba cha ultrasound hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
…………………………..
Madaktari
kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India leo wametembelea Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) kwa lengo la kuangalia mazingira ya kospitali kama
yanaruhusu kuanzishwa huduma za upandikizaji Figo ( Renal Transplant).
Pia,
madaktari hao wametembelea vyumba vya upasuaji, vyumba vya wagonjwa
wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), Maabara Kuu pamoja na Radiolojia.
Daktari
Bingwa wa Mfumo wa Mkojo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Urolojia
MNH Dk. Ryuba Nyamsogoro amesema mbali na hilo pia wataalam hao kwa
kushirikana na watalaam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wataendesha
kambi ya siku mbili kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji wa kuunganisha
mishipa ya damu kwa wagonjwa wanaosafishwa damu (AV Fistula).
‘‘Leo
tutawapitia na kuwandaa wagonjwa wote ambao wanatakiwa kufanyiwa
upasuaji ili kesho tufanye shughuli hii,’’ amesema Dk. Nyamsogoro.
Kambi hiyo itaanza Mei 03 hadi 04, mwaka huu na wagonjwa kati 20 hadi 30 wantarajiwa kufanyiwa upasuaji huo.
No comments:
Post a Comment