Kamanda
wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP
Theopista Mallya akizungumza na wafanyakazi wa Zantel walipomtembelea
katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki
mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya
kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani.
Kamanda
wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP
Theopista Mallya akiwaonyesha wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya
Zantel picha iliyotumwa na wadau wa usalama barabarani inayoonyesha
matumizi mabaya ya barabara yanayofanywa na madereva wazembe.
Wafanyakazi hao walifanya ziara katika kituo cha Polisi cha Oysterbay
jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya kuhitimisha
matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi
duniani. Kushoto ni Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel, Rehema Khalid.
Meneja
wa Afya, Ulinzi na Usalama wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Nashon
Mudala (aliyesimama kulia) akifafanua kuhusu alama muhimu za usalama kwa
wafanyakazi wa Zantel ambazo wanatakiwa kuzizingatia pindi wanapokuwa
kazini wakati wa ziara fupi katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini
Dar es salaam mwishoni mwa juma. Ziara hiyo ilifanywa na wafanyakazi
hao mara baada ya kukamilisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya
Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa
kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista
Mallya, Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel, Rehema Khalid (Kushoto) na
Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.
Askari
wa Usalama barabarani, Wilaya ya Kinondoni S/SGT Rehema (kulia)
akieleza kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wafanyakazi wa Zantel
katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa
wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi ya
kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kushoto ni
Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya
Kinondoni ACP Theopista Mallya na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi
Zantel, Larry Arthur.
Kamanda
wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP
Theopista Mallya (wa pili kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha
Intaneti na Simu wa Kampuni ya Mawasiliano Zantel, Hamza Zuheri
alipotembelewa na wafanyakazi wa Kampuni hiyo katika kituo cha Polisi
cha Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Wafanyakazi hao
walifanya ziara hiyo mara baada ya kuhitimisha matembezi mafupi ya
kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin
akizungumza na wafanyakazi wa Zantel mara baada ya wafanyakazi hao
kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama
mahali pa kazi duniani. Hafla hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya
Kampuni hiyo Msasani jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
No comments:
Post a Comment