Pages

Wednesday, May 31, 2017

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO SHILINGI TRILIONI 11.752


IMG_9376
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihitimisha mjadala wa Bajeti ya Wizara yake ambapo Bunge limepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
IMG_9391
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali za Wabunge wakati wakijadili Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma, ambapo Bunge hilo limepitisha Bajeti ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
IMG_9472
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
IMG_9475
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
IMG_9493
Mkurudenzi wa Idara ya Mipango-Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Richard Mkumbo (kulia), akipongezana na Mkurugenzi wa Bima ya Taifa, kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya wizara hiyo.
IMG_9562
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni nje ya Ukumi wa Bunge mara baada ya Wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
IMG_9599
Gavana wa Benki Kuu (BOT), Prof. Beno Ndullu (kushoto), akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), baada ya Bunge kupitisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Mjini Dodoma
IMG_9613
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akipeana mkono na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Serikali Bw. Mohamed Mtonga, nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
IMG_9659
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoro) akimshukuru na kumpongeza Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kusimamia na kuhakikisha kuwa Bajeti ya Wizara hiyo inaandaliwa kwa viwango vya juu na hatimaye kupitishwa na Bunge Mjini Dodoma ambapo Wizara hiyo imeidhinishiwa kukusanya nakutumia shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
IMG_9716
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa saba kutoka kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Wizara na Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti wa Wizara hiyo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments:

Post a Comment