Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli akiongea machache alipoungana na waumini, ndugu jamaa na
marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa
anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es
salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro,
Dkt. Adelhem Meru. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kardinali
Rugambwa.
Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu
Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la
Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru (kushoto) na Fr. Asis Sylvester
Mendoca (wa pili kulia) wakimsikiliza Fr. Stephano Kaombwe (kulia),
Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay
jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe,
wilayani Temeke, akiongea kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi
wa Kardinali Rugambwa.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu
la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa akiongoza sala wakati wa
hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa
anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es
salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe. Kushoto ni Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli. Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli akisalimiana na masista alipoungana na waumini, ndugu jamaa na
marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe,, Paroko aliyekuwa anahudumu
katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye
sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.
Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli katika picha ya pamoja na waumini, Askofu Msaidizi wa Jimbo
Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, Fr.
Asis Sylvester Mendoca baada ya kuhitimisha hafla ya kumuaga Fr.
Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu
Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la
Chang’ombe, wilayani Temeke.
Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
————————————————————————–
STORY
Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli leo April 2, 2017 ameungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki
kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa
la
Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia
Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke.
Kwenye hafla iliyofanyika
katika ukumbi wa Kardinali Rigambwa na kuongozwa na Askofu Msaidizi wa
Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mama Magufuli
amemtakia kila la heri Fr. Kaombwe katika kituo kipya cha kazi, na pia
amempa salamu toka kwa Rais John Pombe Magufuli ambaye naye amemtakia
heri na fanaka kwa uhamisho huo.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu
la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa alimpongeza Fr. Kaombwe
kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akihudumu katika Paroko hiyo kwa
takriban miaka mitatu na nusu, na pia alitumia nafasi hiyo kumtambulisha
Fr. Asis Sylvester Mendoca ambaye atakaimu nafasi ya Fr. Kaombwe.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei
wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, amempongeza Fr.
Kaombwe kwa mambo mengi aliyoyafanya kanisani hapo, na kwa niaba ya
jumuiya ametoa shukurani nyingi kwa huduma alizokuwa akiwapatia.
No comments:
Post a Comment