Zoezi la kupima uzito kwa ajili ya
pambano kubwa la uzito wa juu duniani katika dimba la Wembley
limekuwa la mvuto mkubwa mno hii leo, kabla ya pambano lao kesho usiku.
Mabondia watakao pambana katika
pambano hilo Anthony Joshua amemzidi uzito kwa tofauti ya kilo 4.5
mpinzani wake Wladimir Klitschko.
Klitschko, raia wa Ukrane ambaye
alitawala uzito wa juu kwa muongo mmoja kabla ya kupigwa na Tyson
Fury, anatarajiwa kutoa upinzani kwa Muingereza Joshua mwenye mkanda
wa IBF.
Anthony Joshua akiwa amenyanyua mkono mmoja juu huku amekunja ngumi wakati akipima uzito
Bondia Wladimir Klitschko akionyesha alama ya vidole viwili wakati wa kupima uzito
Mabondia Anthony Joshua na Wladimir Klitschko wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito
No comments:
Post a Comment