Wananchi
wote mnatangaziwa kuwa kutakuwa na zoezi la kliniki tembezi ya
madaktari bingwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kuanzia
tarehe 3 April 2017 mpaka tarehe 7 April 2017. Madaktari bingwa wa
magonjwa ya akina mama, magonjwa ya macho, magonjwa ya ndani, magonjwa
ya meno, daktari bingwa wa upasuaji, magonjwa ya mifupa, magonjwa ya
mfumo wa mkojo, magonjwa ya masikio, pua na koo na magonjwa ya watoto
watakuwepo kuwahudumia kwa gharama nafuu sana. Wote mnakaribishwa na
atayeona tangazo hili tafadhali mjulishe na mwenzako. Tangazo hili pia
linapatikana katika tovuti rasmi ya mkoa wa Singida, bonyeza www.singida.go.tz sehemu ya matangazo utaliona.
No comments:
Post a Comment