Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt.Kijaji |
Mikoa mitatu ya Tanga, Morogoro
na Iringa, imenufaika na kiasi cha shilingi bilioni 6.5 zilizotolewa
kama mkopo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) tangu benki hiyo
ianzishwe mwaka 2015.
Kauli
hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu swali na msingi lililoulizwa
na Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Felister Aloyce Bura, aliyetaka
kufahamu ni lini Serikali itaanza kutoa huduma kwa wakulima wadogo
wadogo wa mkoa wa Dodoma.
Dkt.
Kijaji ameeleza kuwa hadi kufikia mwezi Desemba, 2016, TADB imetoa
mikopo ya jumla ya shilingi 6,489,521,120 kwa ajili ya kutekeleza miradi
ishirini (20) ya kilimo katika mikoa hiyo mitatu ya Iringa, Morogoro na
Tanga.
“Sambama
na utoaji mikopo, Benki inatoa mafunzo kwa wakulima ambapo hadi sasa
vikundi 336 vya wakulima wadogowadogo vyenye jumla ya wanachama 44,400
wamepatiwa mafunzo hayo katika mikoa hiyo mitatu” aliongeza Dkt. Kijaji
Amesema
kuwa Benki hiyo inatarajia kuanza kutoa huduma hiyo kwa wakulima
wadogowadogo wa Mkoa wa Dodoma na mikoa mingine jirani wenye sifa.
“Benki
imepata nafasi kwa ajili ya kufungua ofisi katika jengo la PSPF mjini
Dodoma na itakabidhiwa ofisi hiyo mwezi Julai, 2017, baada ya mkandarasi
kukamilisha ujenzi wa jengo hilo” Alisisitiza Dkt. Kijaji
Dkt.
Kijaji amesema kuwa tayari Benki hiyo imemwandikia barua Katibu Tawala
wa mkoa wa Dodoma ili kuomba aipatie miradi mizuri ya kilimo ambayo mkoa
unapendekeza Benki iifikirie katika zoezi la kutoa mikopo itakayoanza
kutolewa mwishoni mwa mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment