Pages

Thursday, March 30, 2017

ZANTEL YATOA MSAADA WA VITABU 152 KWA CHUO CHA KARUME CHA SAYANSI NA UFUNDI CHA UNGUJA,ZANZIBAR


 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour (kushoto) akisaini kitabu cha wageni baada
ya kuwasili kwenye Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi katika hafla ya kukabidhi vitabu 152 vilivyotolewa na Zantel kwa Chuo hicho. Kulia ni Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren. Hafla hiyo ilifanyika juzi kisiwani
Unguja.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi wakishuhudia hafla ya kukabidhiwa
msaada wa vitabu zaidi ya 152 kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika juzi kisiwani Unguja.
 Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren (wa pili kushoto) akikabidhi vitabu kwa Mkuu wa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi, Haji Abdulhamid. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin wakishuhudia.
Mkuu wa Chuo cha Karume cha Sayansi na ufundi Haji Abdulhamid akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa vitabu 152 vyenye thamani ya Tsh 10 milioni kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Kushoto ni Mkurugenzi wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour, Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin.

No comments:

Post a Comment