Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Elimu ya Watu wazima Tanzania Dkt. Fidelice Mafuniko akisisitiza jambo
kabla ya kusainiana hati za makubaliano kati ya Taasisi hiyo na Shirika
lisilo la Kiserikali la Marafiki wa Watoto wanaoishi na ugonjwa wa
Saratani ili kuimarisha uhusiano utakaosaidia kuwapa fursa ya elimu
watoto waliopo Hosipitalini wakisumbuliwa na ugonjwa huo ili kuwapa haki
sawa na wale walio katika mfumo rasmi.kulia ni Mkurugenzi wa shirika
hilo Bw. Walter Miya.
Mkurugenzi wa shirika Shirika
lisilo la Kiserikali la Marafiki wa Watoto wanaoishi na ugonjwa wa
Saratani Bw. Walter Miya (kulia) akizungumza kuhusu umuhimu na Faida za
Shirika hilo kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuwawezesha kielimu
watoto wanaougua ugonjwa wa Saratani.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Elimu ya Watu wazima Tanzania Dkt. Fidelice Mafuniko (kulia) na Meneja
wa mradi wa Elimu toka Asasi ya Kimataifa ya BRAC Maendeleo Tanzania
Bw.Abdullah Mahtab wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano
utakaowezesha wasichana waliokosa fursa hiyo katika mfumo rasmi kupata
elimu kupitia mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Elimu ya Watu wazima Tanzania Dkt. Fidelice Mafuniko (kulia) na Meneja
wa mradi wa Elimu toka Asasi ya Kimataifa ya BRAC Tanzania Bw.Abdullah
Mahtab wakibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano mara baada ya
kusaini makubaliano ya ushirikiano.
Mkurugenzi wa Asasi ya Marafiki wa
watoto wanaoishi na saratani Bw. Walter Miya (kulia) akibadilishana
hati za makubaliano ya ushirikiano na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya
watu wazima Dkt. Fidelice Mafuniko.
(Picha na Frank Mvungi Maelezo)
……………………
Frank Mvungi-Maelezo
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
imejidhatiti kuwawezesha wasichana waliokosa Elimu ya
Sekondari katika
mfumo rasmi kutokana na kupata Mimba na Umasikini ili waweze kushiriki
katika ujenzi wa Taifa kwa kuwajengea mazingira ya kupata elimu nje ya
mfumo rasmi.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Fidelice Mafuniko
wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano baina ya
Taasisi hiyo na Asasi ya Kimataifa ya BRAC Maendeleo Tanzania pamoja na
Marafiki wa Watoto wanaougua Saratani.
Akizungumzia Makubaliano hayo Dkt.
Mafuniko amesema utekelezaji wa awamu ya kwanza ya majaribio ya mradi
wa kuwawezesha wasichana yalikuwa ya miaka 2 kuanzia June 2014 hadi
Machi 2016 ambapo mradi ulitekelezwa katika Mikoa ya Dar es Salaam,
Singida,Shinyanga,Mwanza,Tabora na Tanga.
Katika mradi huo jumla ya
wasichana 1,950 wamenufaika na mpango huo kwa kupata elimu ya Sekondari
kwa njia ya ujifunzaji huria na masafa katika hatua ya kwanza
nakuongeza kuwa awamu ya pili itahusisha walengwa 300 kutoka Mkoa wa
Tanga ambao tayari wameshasajiliwa.
Awamu ya Tatu inaanza kuteklezwa
kuanzia sasa kwa kipindi cha Miaka 3 na itahusisha wasichana takribani
2000 kutoka katika Mikoa ya Dar es
Salaam,Singida,Shinyanga,Mwanza,Tabora na Tanga.
Mradi huu unatarajia kupanuka zaidi na kuwafikia walengwa wengi zaidi katika mikoa ya Pembezoni ikiwemo Kigoma,Rukwa na Ruvuma.
Kwa upande wake Meneja wa Elimu
kwa Umma kutoka Asasi ya Maendeleo ya BRAC Tanzania Bw. Abdullaah Mahtab
Khan amepongeza mpango huo na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Taasisi
hiyo na Asasi yake na kutaka uendelezwe kwa manufaa ya Watanzania.
Naye Mkurugenzi wa Asasi ya
Marafiki wa Watoto wanaougua Saratani Bw. Walter Miya amesema kuwa asasi
yao inatekeleza mradi wa kuwawezesha watoto wanaougua Saratani kielimu
ambapo hospitali 16 zinatumika.
Alitoa mfano kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo wanafanya kazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
“Asasi yetu imejipanga
kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kuwawezesha watoto wenye
saratani kupata Elimu kwani huu ni wajibu wetu sote kama Watanzania”
Alisisitiza Miya.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
(TEWW) ilianzishwa mwaka 1960,Pamoja na majukumu mengine ina jukumu la
kuratibu na kutoa Elimu ya Sekondari kwa Vijana na Watu Wazima walio nje
ya Shule wenye uhitaji na waliokosa elimu hiyo.
No comments:
Post a Comment