NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai amewasihi vijana wa
Chama hicho kuwania nafasi za uongozi katika ngazi za mashina hasa
Ubalozi wa Nyumba kumi ili kuongeza nguvu za kiutendaji katika ngazi
hizo.
Amesema
nafasi hizo kwa kiwango kikubwa zimekuwa zikishikiliwa na Wazee ambao
umri wao hauwaruhusu kuendelea kuhudumu katika uwanja wa mapambano ya
kisiasa kwa sasa.
Akizungumza
Naibu Katibu Mkuu huyo na viongozi, Watendaji na Wanachama wa Jimbo la
Jang’ombe katika mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa Chama
iliyofanyika katika Tawi la CCM Matarumbeta Unguja.
Vuai
alisema nguvu za taasisi hiyo zinaanzia katika ngazi za chini za
uongozi zinazotakiwa kusimamiwa na viongozi vijana wenye uwezo wa
kupigania maslahi taasisi hiyo bila ya woga.
“
Kwa miaka mingi kila ukifika uchaguzi wa Chama na Jumuiya zake
wanaojitokeza kuwania ngazi za ubalozi wa nyumba kumi ni Wazee na watu
ambao umri wao unaelekea katika utu uzima, ambapo vijana mnazikimbia
nafasi hizo na kugombea nafasi za juu wakati ngazi za
chini hazina watu
wenye nguvu wa kuzisimami”.alisisitiza Vuai na kuongeza kuwa mtaji wa
kisiasa wa CCM ni wanachama hai wanaopatikana kupitia ngazi za Matawi na
Mashina.
Alieleza
kuwa Wazee kwa sasa wanatakiwa kupumzika huku wakipewa fursa za
kushauri masuala mbali mbali ya kisiasa ndani ya taasisi hiyo, kwani wao
ndio mashujaa wanaostahiki kupewa heshima kutokana na mshango wao wa
kufanya mapinduzi ya mwaka 1964 yaliyoleta ukombozi wa kudumu kwa
Wazanzibar.
Aliwashauri
wanachama hao kuwachagua viongozi imara wenye uwezo wa kupanga na
kusimamia mikakati endelevu ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa Dola
mwaka 2020.
Sambamba
na rai hizo alitoa tahadhari kwa viongozi, watendaji na wanachama wa
chama hicho kuepuka mbinu na propaganda za wapinzani kwani historia ya
siasa za Zanzibar zinathibitisha njama zinazofanyika hivi sasa
kuiangamiza CCM zimewahi kutumika kuihujumu Afro Shiraz Party (ASP)
mwaka 1959.
Hata
hivyo alisema mipango ya kuimarisha CCM katika jimbo hilo iendane na
dhana ya siasa na uchumi kwa kutekeleza miradi mbali mbali ya
kimaendeleo itakayosaidia shughuli za kiutendaji.
Aidha
aliwakumbusha wafuasi wa Chama hiocho kutokubali kuwapokea Watu
wanaohamia katika Jimbo hilo kinyume na sheria za Uhamiaji kwani baadhi
yao wanapandikizwa na vyama vya upinzani kwa nia ya kujiandisha kupata
ZAN ID ili wajiorodheshe kwenye daftari la wapiga kura katika maeneo
yasiyokuwa halali kwao kisheria.
Naye
Kaimu Katibu wa Jimbo hilo Nd. Said Bakar akisoma risala ya maendeleo
na hali ya kisiasa alisema toka kumalizika kwa uchaguzi wa marudio CCM
imekuwa ikikubalika kwa wananchi kutokana na utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya mwaka 2015/2020 kwa wananchi wote.
Wakizungumza
wafuasi hao kwa nyakati tofauti wameahidi kuzifanyia kazi kwa vitendo
nasaha zilizotolewa na viongozi wa ngazi za juu za chama hicho.
Hata
hivyo walielezea kukerwa na tabia za upotoshaji wa taarifa za viongozi
wa umma katika mitandao ya kijamii na kuiomba CCM ishauri serikali
iwatafute watu wanaomiliki mitandao hiyo ili wafikishwe katika vyombo
vya kisheria.
No comments:
Post a Comment