Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe,
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mbunge wa Kyela , ameshudia zoezi
la kuingizwa majini kwa Meli mpya ya pili ya mizigo iitwayo MV Ruvuma
kwenye bandari ya Itungi, Wilayani Kyela.
Tukio hilo la
kuiingiza Meli hiyo making limefanyika Machi Mosi . Meli hiyo yenye
uwezo wa kubeba mzigo zaidi ya tani 1000 inaungana na Meli nyingine mpya
MV Njombe yenye uwezo wa kubeba zaidi ya tani 1000 ambayo iliingizwa
majini siku tano zilizopita. Meli zote mbili zipo kwenye hatua ya mwisho
ya utengenezaji na majaribio kabla hazijaanza rasmi kubeba mizigo
kwenye ziwa Nyasa.
Tayari wateja
mbalimbali wamejitokeza kutaka mizigo yao ianze kubebwa yakiwemo
makampuni yanayojishughulisha na biashara ya makaa ya mawe.
No comments:
Post a Comment