Kamanda
wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Mkumbo akionyesha
silaha mbalimbali zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika wilayani
Ngorongoro iliyofanyika wiki mbili zilizopita.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akionesha
waandishi wa habari baadhi ya silaha zilizopatikana katika operesheni
iliyofanyika wilayani Ngorongoro.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Arusha akiwaonesha waandishi wa habari moja ya silaha
ya kivita aina ya Chinese 56 Sub Machine Gun (SMG) iliyopatikana kwenye
operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro.
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi
la Polisi mkoani hapa limefanikiwa kupata jumla ya bunduki kumi za aina
nne tofauti zikiwemo Sub-Machine Gun sita baada ya operesheni ya wiki
mbili iliyoanza tarehe 15.02.2017 katika wilaya ya Ngorongoro.
Akitoa
taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo asubuhi, Kamanda wa Polisi
mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema silaha hizo
zilipatikana katika vijiji vya Olorieni Magaiduru, Oldonyosambu na Sale
vilivyopo katika tarafa za Loliondo na Sale.
Alisema
mafanikio hayo yalitokana na taarifa fiche ambazo zilibainisha kwamba
kuna baadhi ya watu wanamiliki silaha za kivita hivyo mahojiano makali
baina ya askari wa Jeshi la Polisi na Viongozi wa Kimila na kuwataka
wasalimishe silaha popote pale ambapo walikuwa wanaamini kwamba silaha
hizo zitawafikia Jeshi la Polisi.
Akibainisha
vijiji ambavyo silaha hizo zilipatikana kuwa ni Olorieni Magaiduru
zilipatikana silaha aina ya Chinese 56 SMG moja yenye namba MT. 70B 1
2730021 na risasi 21 pamoja na silaha aina ya Semi Automatic Rifle
(S.A.R) yenye namba KN 250374 ikiwa na risasi nne.
Katika
kijiji cha Oldonyasambu ilipatikana silaha aina ya Mark IV yenye namba
ZKK 5602 pamoja na silaha nne aina ya Chinese 56 Sub-Machine Gun (SMG)
zikiwa na risasi 19. Silaha hizo nne ni Chinese 56 SMG yenye namba RT
7663, bunduki ya pili namba yake ni 563631144 na bunduki mbili nyingine
hazikuwa na namba.
Kamanda
Mkumbo alisema katika kijiji cha Sale silaha aina ya Chinese 56 SMG
yenye namba 89020539 ikiwa na risasi 15 kwenye magazine ilipatikana
pamoja na silaha nyingine mbili tofauti ambazo ni S.A.R yenye namba
25032534 na Mark III yenye namba 263126.
Aidha
kamanda Mkumbo aliwataka wananchi wanaomiliki silaha za moto kinyume
cha sheria wazisalimishe mara moja kwenye ofisi za mitaa, vijiji na hata
vituo vya Polisi vyovyote vilichopo karibu huku akitoa onyo kwa wale
ambao watakaidi na wakikutwa nazo hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yao. Alisema Operesheni hiyo ni endelevu na itakuwa katika maeneo
tofauti ya mkoa huu na si wilaya ya Ngorongoro pekee.
No comments:
Post a Comment