Mkurugenzi wa halmashauri ya
Ileje Haji Mnasi akiwa kwenye harambee ya uchangiaji wa vifaa vya ujenzi
wa zahanati ya ushirika wa Rungwa iliyopo katika wilya ya Ileje.
Mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Ileje Haji Mnasi alihesabu kiasia cha shilingi milioni nne na
zaidi kwa lengo la ufanikishaji wa upatikanajiwa vifaa vya kumalizia
ujenzi wa zahanati ya ushirika wa Rungwa.
Na fredy Mgunda.
Mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Ileje Haji Mnasi afanikisha azima ya ujenzi wa zahanati bora
katika ushirika wa rungwa kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa
wananchi wa wilaya ya Ileje.
Akizungumuza wakati wa harambee ya
kuchangia ujenzi wa zahanati hiyo mkurugenzi Mnasi alisema kuwa
wameamua kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kuendelea kuboresha hutuma za afya kwa wananchi ili wafanye
kazi kwa kujituma.
“Kauli mbiu ya Rais wetu ni hapa
kazi tu sasa ukiwa na jamii ambayo dhohofu huwezi kufikia malengo ya
hapa kazi hivyo nimefanya harambee hii kumuunga mkono Rais kwa kuboresha
huduma za afya katika wilaya yetu ya Ileje na kuwafanya wananchi
kufanya kazi kwa kujituma huku wakiwa na afya njema na kuendelea
kulijenga taifa kwa kufanya kazi kwa kujituma”.alisema Mnasi
Mnasi alisema wananchi wanatakiwa
kujitoalea kwa hali na mali kufanikisha ujenzi wa zahati hiyo
unakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa jamii.
“Leo hii tumefanya harambee ya
kuchangia kupatikana kwa vifaa vya kumalizia ujenzi wa zahanati
unaogharimu kiasi cha shilingi milioni sita na nashukuru mungu
nimefanikiwa zaidi kupata shilingi milionii nne hivyo lengo limetimia
kilicho baki ni utekelezaji tu labda niwaombe kuzitumia pesa hizi vizuri
kununua vifaa ya ujenzi ili wananchi waanze kupata huduma bora”.
Alisema Mnasi
Aidha Mnasi alizitaka taasisi
nyingine kuiga mfano wa ushirika wa Rungwa kwa ujenzi wa zahanati hiyo
ambayo itarahisisha uwepo wa huduma bora kwa jamii husika.
“Tuna taasisi nyingi sana katika
wilaya yetu hivyo naziomba nazo zijitahidi kuwa na malengo ya ujenzi wa
zahanati ili kuendeleza kutoa huduma bora kwa jamii na kuifanya jamii
kuwa huru kufanya kazi kwa nguvu huku wakiwa na afya bora”.alisema Mnasi
Nao baadhi ya waumini wa ushirika
wa Rungwa walimushukuru Mkurugenzi huyo kwa kuendelea kujituma kufanya
kazi kwa wananchi wa chini na kuwaboresha huduma za afya.
“Tulikuwa tunahitaji zaidi ya
milioni sita lakini uwepo wa mkurugenzi Mnasi katika harambee ya leo
kumesaidia kupata pesa nyingi ambazo zimefanisha azma ya umaliziaji wa
ujenzi wa zahanati yetu”.walisema washirika
No comments:
Post a Comment