Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) limeahidi kuendelea kuzisaidia redio jamii kwa
lengo la kuhakikisha sauti za wanyonge zinapazwa na kusikika ili kukuza
demokrasia nchini.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii
Tanzania (COMNETA), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema UNESCO alisema kuwa wakati umefika
kwa wadau wa sekta ya habari kufikiri kwa kina namna ya kuhabarisha umma
kwa kuangalia namna ya uwasilishaji ambapo kwa sasa changamoto kubwa ni
kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na namna ambapo redio zinaweza
kushindana na vyombo vingine.
Alisema kwa wanahabari wanapaswa kuwa makini na taarifa wazitoazo kwa
jamii kwani kumekuwa na mazoea ya baadhi yao kuripoti habari bila
kufanya uchuinguzi wa kina huku wakitumia chanzo kimoja cha habari
badala ya kujiuliza maswali mengi ili kupata taarifa sahihi.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari
wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay akizungumza machache
wakati wa mkutano mkuu wa wajumbe wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya
Habari Jamii Tanzania (COMNETA) unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu
Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Aliwashauri wanachama wa COMNETA, wawe
na umoja, mshikamano na kupendana ili kuepuka migogoro inayoweza
kuyumbisha ustawi wa mtandao huo. “Ninawaomba sana, COMNETA, muwe mfano
wa kuigwa kwa kuepuka migongano ya wenyewe kwa wenyewe ikiwamo kugombea
madaraka ili kuwa umoja wa mfano kwa katika tasnia ya vyombo vya habari
hapa nchini’.
‘Vipindi mbalimbali vya kuhamasisha
maendeleo vinavyorushwa na redio hii vimesaidia sana kuhamasisha
wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa mkubwa hapo Micheweni”
alisema Zulmira Rodrigues
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
COMNETA, Mohamed Tibanyendera akizungumza na wadau mbalimbali wa vyombo
vya habari jamii waliokutana kwenye mkutano mkuu ili kujadili changamoto
na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya uliodhaminiwa na Shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya
Habari Jamii Tanzania-COMNETA, Prosper Kwigize alisema kuwa ipo
changamoto kwa baadhi ya maafisa habari mikoani na wilayani kuleta
urasimu mkubwa katika utoaji wa taarifa zinazohitajika kwa waandishi wa
habari hivyo kukwamisha upatikanaji wa habri kwa umma. Pia kuna
changamoto mbalimbali kwenye chama hicho hivyo ni vyema kuzitafutia
suluhiso la msingi ili mtandao huwe imara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
COMNETA, Mohamed Tibanyendera alisema kuwa kwa siku za nyuma redio
ilikuwa ni chombo cha kuaminika katika utoaji wa habari hivyo kujijengea
umaarufu na kuaminika zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo kuna
upotoshaji mkubwa. Pia aliweza kuyatolea majibu maswali yaliyoulizwa na
wajumbe wa bodi ya COMNETA ili kuimarisha uwajibikaji katika Mtandao wa
Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo
vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Prosper Kwigize akizungumza na
viongozi wa vyombo vya habari jamii wakati wa mkutano mkuu wa COMNETA
unaondelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Bodi ya Udhamini ya COMNETA, Balozi Christopher Liundi akizungumza
jambo wakati wa mkutano mkuu Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania
(COMNETA) unaofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam chini ya udhamini wa UNESCO.
Katibu
wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Marco
Mipawa akisoma marejesho kwenye mkutano mkuu unaondelea OUT jijini Dar
es Salaam.
Pichani
juu na chini ni Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya COMNETA ambao pia ni
Mameneja na wawakilishi wa vituo vya redio jamii nchini wakishiriki
kutoa maoni kwenye mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea katika ukumbi wa
Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Kutoka
kushoto ni Afisa Programu wa Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Nancy
Kaizilege na Mkufunzi wa Redio Jamii UNESCO, Rose Haji Mwalimu
wakirekodi mambo muhimu katika mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea
jijini Dar es Salaam.
Timu ya Azania Group, ndiyo
itakayowakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda ya Afrika
Mashariki, ya Benki ya “Standard Chartered-Road to Anfield”
yatakaofanyika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jumamosi, Machi 4.
Azania walipata ushindi huo kwa kuichakaza timu ya H&R Consultancy
mabao ya 6-5 kwa penati dhidi ya katika mchezo wa kukata na shoka
uliofanyika mwishoni mwa wiki na kufanikiwa kuipeperusha bendera ya
Tanzania.
Kwa maana hiyo, Azania Group wanatarajia kumenyana uso kwa uso na
washindi wa michuano hiyo kutoka nchi za Kenya na Uganda.
Washindi wa michuano hiyo nchini Uganda ni timu ya Cocacola wakati
kidedea wa kombe hilo nchini Kenya ni Radio ya Capital FM.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard
Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano na
Masoko wa Benki hiyo, Juanita Mramba wakikabidhi kikombe kwa Bw Sikaba
Hamisi ambaye ni Nahodha wa timu Azania Group, Mshindi wa kitaifa wa
mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield),
mashindano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya JK Youth
Park, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa habari muda
mfupi baada ya kutwaa ushindi huo, Nahodha wa Azania Group, Bw. Shabaka
Hamisi alisema maandalizi yao mazuri ndiyo siri ya ushindi wao na
kuongeza kwamba wapo tayari kuwanyoa hao wageni asubuhi kabisa.
“Katika jambo lolote kama unataka kufanya vyema, maandalizi mazuri
yanasaidia sana. Kwa upande wetu, tulifanya mazoezi yakutosha na ndiyo
maana leo tumeibuka washindi.” Alisema.
Aliongeza, “Siyo kwamba wenzetu walikua wabovu, ila umakini na utulivu
kwa upande wa wachezaji wangu ndiyo kilichotusababishia kupata matokeo
mazuri.”
Alisema mazoezi ya kujipanga kwa ajili ya mechi tayari yameshaanza kwa
ari na nguvu mpya, akiongeza kuwa ushindi kwao ni lazima.
Kwa upande wake, Phillip David, nahodha wa H&R Consultancy alisema
kukosekana kwa ukosefu wa umakini katika ushambuliaji ndiyo
uliosababisha timu yake kupoteza mechi hiyo, hata hivyo alishukuru kwa
kuibuka mshindi wa pili wa mashindano hayo.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard
Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano na
Masoko wa Benki hiyo, Juanita Mramba (kulia) wakifurahi katika picha ya
pamoja na timu ya Azania Group wakikabidhi kikombe kwa timu Azania
Group,Mshindi wa kitaifa wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered
2017(Road to Anfield), mashindano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye
viwanja vya JK Youth Park,Gerezani jijini Dar es Salaam.
“Kama ulivyoona, mechi ilikuwa moja moja
hadi tukaingia kwenye matuta. Wenzetu walipata penati sita wakati sisi
tulifunga tano. Nafasi ya kushinda ilikuwa upande wetu lakini Mungu
hakupenda iwe ivyo,” alisema.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Limited, Sanjay
Rughani aliwaasa wachezaji wa Azania Group kuwa wajiandae kikamilifu ili
waubakishe ubingwa nchini Tanzania.
“Sisi hakuna zawadi nzuri ambayo tunaitaka kutoka kwenu zaidi ushindi.
Fanyeni mazoezi ya kutosha ili Jumamosi inayokuja muweze kushinda mechi
zenu zote dhidi ya hizo timu kutoka Kenya na Uganda. Na sisi kama
wadhamini tutakua pamoja nanyi ili kuhakikisha kwamba mnapata ushindi
hapa nyumbani,” alisema Sanjay.
Naye Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Benki hiyo, Juanita Mramba,
aliwapongeza kwa ushindi huo lakini akiwatahadharisha kuwa safari yao
ndiyo kwanza imeanza.
“Leo mmeshinda mashindano haya, Jumamosi kazi yenu ni kubwa zaidi kwani
mtacheza na wageni wawili, hivyo jipangeni vizuri zaidi mkiutumia vyema
uwanja wa nyumbani,” alisema.
Ukiachia mbali Azania ambao waliondoka na kombe za dhahabu, washindi wa
pili H&R Consultancy walijitwalia kombe la shaba, huku washindi wa
tatu PWC wakitwaa kombe la Bronze.
Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto)
akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya HR Consultants, Phillip David
ambao ni washindi wa pili wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered
2017 (Road to Anfield), yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja
vya JK Youth Park, Gerezani jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio
hilo ni Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael
Shio (kulia).
WAZIRI wa Kilimo ,Chakula,Mifugo na Uvuvi Dk.
Charles Tizeba (pichani), anatarajia kufungua kongamano la siku tatu la wadau wa sera za kilimo kesho jijini
Dar es Salaam.
Aidha, kongamano hilo litahudhuriwa na wadau zaidi
ya 200 kutoka nchi mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Mwenyekiti wa Kampuni ya
Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF), Audax Rukonge, alisema serikali
imekusudia kuweka kipaumbele kwenye viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo.
Kongamano hilo litalenga kuongeza uelewa
miongoni mwa watunga sera kuhusu mchango wa kilimo katika kuhamasisha ukuaji wa
viwanda Tanzani.
“Wadau watajadili kupata tafsiri halisi ya sekta ya
uchakataji mazao ya kilimo katika muktadha wa mageuzi ya viwanda Tanzania,”alisema
Rukonge alisema kongamano hilo limedhaminiwa na
USAID, Benki ya Dunia,ANSAF,JICA na wadau wengine ambao wamesaidia kuleta
watalamu wakiwamo wakulima, watafiti,wafanyabiashara na watunga sera.
Mratibu wa Jukwaa la Sera ya Kilimo na Mchumi
mwandamizi Wizara ya Kilimo, Sophia Mlote alisema kongamano hilo la tatu
litajadili maendeleo ya kilimo nchini ikiwamo kujadili namna ya kutetea
sera,sheria,kanuni.
Pia alisema kongamano hilo litajikita katika
kujadili juu ya mpango wa kilimo cha mihogo,mikunde, samaki, mazao,
usafirishaji pamoja na vifungashio kwa kuwa wazalishaji wengi hawana
vifungashio.
Kiongozi wa band ya East African Ngwasuma Original Band Kingombe
Blaise wa pili kulia akiwa anafanya mambo katika ukumbi wa Filomena
Bar uliopo Boma Ngo'mbe mkoani Kilimanjaro wakati wa onyesho lao
walilofanya mwishoni mwa wiki hii
Waimbaji
na wanenguaji wa bendi ya East African Ngwasuma Original Band wakiwa
wanawapagawisha wakazi wa Bomang'ombe na mitaa yake
wanenguaji wa band ya East African Ngwasuma Original Band wakiwa wanaonyesha viuno ikiwa wanacheza staili yao mpya ya Kampa Kampa tena
Rappa anaejulikana kwa jina la Papii katalogi akifanya yake ndani ya ukumbi wa Filomena Bar mkoani kilimanjaro
Habari picha na Woinde Shizza,Kilimanjaro
Bendi mpya iliongia mjini kwa kasi inayoongozwa na msanii maarufu Kingombe Blaise imewapagawisha wakati wa mji wa BomaNg'ombe na vitongoji vyake mara baada ya kutoa burudani kali ambayo iliacha historia
Bendi mpya iliongia mjini kwa kasi inayoongozwa na msanii maarufu Kingombe Blaise imewapagawisha wakati wa mji wa BomaNg'ombe na vitongoji vyake mara baada ya kutoa burudani kali ambayo iliacha historia
Wakiongea
na blog hii baadhi ya washabiki wa mziki wa dance walisema kuwa
wamefuarahi sana kupewa burudani na bendi hiyo , kwani walikuwa walikuwa
na kiu ya mda mrefu kupata burudani kama hii
Mmoja
wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Pendo Petro alisema kuwa
bendi hii iko vizuri na imewapa burudani nzuri hivyo wanaiombea iendelee
kudumu ili wao kama wananchi wa mkoa wa kilimanjaro waweze kuendelea
kupata burudani
Akiongelea
onyesho hilo kiongozi wa bendi hiyo Kingombe Blaise alisema kuwa wao
wamejipanga kuwapa burudani ya kutosha wakazi wa mkoa wa Arusha ,moshi
naTanzania kwa ujumla
"sisi
tumejipanga kuwapa burudani wapenzi wa mziki wa dance na kwa sasa
tunafanya hizi show ila tunampango wa kuzindua Albamu yetu hivi karibuni
na muda ukifika atutaacha kuwaaambia wapenzi wetu wa muziki huu ili nao
waweze kutusapoti na tunawaaidi tutawapa burudani ya kweli ambayo kila
mmoja ambaye anajua mziki wa dance ataifaurahia"alisema Kingblez
Aidha
alisema kuwa pamoja kunaushindani mkubwa katika muziki huuu wao
hawatetereki maana wanaamini kabisa amna bendi ambayo inawafikia kwa
kutoa burudani hivyo wapenzi wa mziki wa dance waendelee kusubiri na
waendelee kuwapa ushirikiano ili watimize malengo yao ya kuwapa burudani
.
Mstahiki Meya wa Jiji la
Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi akisisitiza jambo kwenye kikao cha baraza
la madiwani leo kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la
Tanga,Daudi Mayeji kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Kassim
Mbughuni
Naibu Meya wa Jiji la
Tanga,Mohamed Haniu akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la
Madiwani
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji |
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akizunguza kwenye kikao cha baraza la Madiwani leo kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Kassim Mbughuni |
Baadhi ya Wataalamu wa
Halmashauri ya Jiji la Tanga nao wakiwa makini kuchukua baadhi ya hoja
zilizokuwa zikiwasilishwa na madiwani kwenye kikao hicho cha baraza la
madiwani
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim akifuatilia kwa umakini kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Halmashauri Jijini Tanga. |
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia
kwa umakini kikao hicho kulia ni Diwani wa Kata ya Central Jijini
Tanga,Khalid Mohamed wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri
ya Jiji la Tanga wa kwanza kulia ni Mratibu wa Ukimwi Jiji la
Tanga,Moses Kisibo anayefuatia ni Meneja Mkuu wa kituo cha Television ya
Jiji la Tanga (TATV) Mussa Labani wakifuatilia kwa umakini majadiliano
ya kikao hicho
Baadhi ya Madiwani
wakifuatilia kwa umakini kikao hichoMbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea mara baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Madiwani.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga (CCM).Alhaji Mustapha Selebosi kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji nyuma yao ni Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu mara baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Madiwani leo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Hii ndiyo transfoma kubwa iliyolipuka huko Buguruni jijini Dar es Salaam
Shirika
la Umeme Tanzania, (TANESCO), linapenda kuutaarifu umma kuwa Jumapili ya tarehe
26/02/2017 majira ya saa kumi alasiri kulitokea moto katika chumba cha
transfoma kubwa iliyopo eneo la Tazara (Buguruni Substation) na kusababisha
kuungua kwa Transforma kubwa ya Buguruni (15mva, 33/11kv) na hivyo kusababisha
maeneo ya Vingunguti, Kiwalani, Baadhi ya viwanda viliyopo barabara ya Nyerere
na maeneo yaliyo jirani na haya kukosa Umeme. Kazi bado inaendelea na pindi
itakapokamilika Umeme utarejea katika hali yake ya kawaida. Baada ya kutokea
kwa moto huo jitihada za kuuzima zilianza ikiwa ni pamoja na kuwapigia simu
"fire" ambao walifanikiwa kuuzima moto huo ambao ulikuwa umeshaharibu
transforma hiyo kwa kiasi kikubwa. Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wote
unaoendelea kujitokeza.
Mshiriki wa Tigo half Kilimaratho mwenye miaka 90, Joram Zacharia Mollel baada ya kumaliza mbio hizo za kilomita 21, Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini |
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadick akimpa tuzo mshiriki wa Tigo half Kilimaratho mwenye miaka 90, Joram Zacharia Mollel baada ya kumaliza mbio hizo za kilomita 21 |
Washindi wa riadha ya kilomita 21 iliyofadhiriwa na Tigo kwenye Kilimarathon wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali. |
Mbunge
wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akikinga maji kwenye ndoo kuashiria sasa kisima cha maji
kimefunguliwa na kuanza kutumia kwa wakazi wa mtaa wa Igungandembwe
manispaa ya Iringa akiwa na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove wakati
wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mbunge
wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa kujimba visima ambaye
pia ndiye aliyechimba kisima hicho.
Mbunge
wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akiangalia maji waliyokuwa wanatumia wananchi mtaa wa
Igungandembwe manispaa ya Iringa.
Mbunge
wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akiangalia maji waliyokuwa wakitumia wananchi wa mtaa huo
Na haya ndio maji waliyokuwa wanatumia wananchiwa mtaa wa Igungandembwe
manispaa ya iringa kabla ya kujimbiwa kisima
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wananchi wa mtaa wa Igungandembwe
manispaa ya iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta
Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na diwani wa kata ya Nduli Bashir
Mtove kwa msaada wa kuwachimbia kisima cha maji safi na salama.
Wakizungumza na blog hii
wananchi hao wamesema kuwa wanatakribani miaka hamsini na tatu (53) hawajawahi
pata maji masafi na salama.
“Angalia maji haya machafu
ndio tulikuwa tunakunywa na kupikia ila mungu alikuwa anatusaidia tu kutuepusha
na magonjwa mbalimbali kiukweli leo tunafuraha sana kuanza kutumia haya maji na
ndio maana unaona wananchi wanafuraha nawameanza kunywa maji hapa hapa kwenye
kisima hiki kwa kuwa bado hawaamini kilichotokea”,walisema wananchi.
Wananchi wao wamemuomba
mbunge Ritta kabati na Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove kuendelea kutatua
changamoto za wananchi kwa kuwa walichaguliwa na wananchi kwa lengo la
kuwatumikia.
Kwa upande wake mbunge wa
viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
alisema kuwa wataendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa kuwa
yeye ni mbunge wa wananchi wote bila kubagua vyama.
Kabati alisema kuwa
ataendelea kuwachimbia visima na kukarabati majengo ya shule zilizochakaa
katika mkoa wa Iringa kwa kuwa yeye ni mbunge wa mkoa wa Iringa hivyo aliwaomba
wananchi kuendelea kuiamini serikali ya chama cha mapinduzi kwa kazi kubwa
wanayoifanya kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
Magufuli.
“Hivi hamuoni nimeamua kufika huku ambako hata
viongozi wengi hawajafika ila mimi nimekuja nimewaleta kisima na maji safi na
nitaendelea kuja kutatua matatizo ya mtaa huu kwa kuwa tumetumwa na Rais
kufanya kazi kwa wananchi wa chini ndio maana hata mimi nimeanza kufanya kazi
huku mbali japo kuwa ndio jadi yangu kuwatumikia sana wananchi wa chini sasa
naombeni mniunge mkono katika juhudi zangu za kuwaletea mandeleo”.alisema
Kabati
Aidha Kabati alisema kuwa
lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuleta maendeleo kuanzia huku chini
kupanda juu hivyo tufanye kazi kwa kujituma ili tuende sambamba na kasi ya Rais
wetu.
Naye Diwani wa kata ya nduli
Bashir Mtove alimshukuru mbunge huyo kwa jihada zake za kuleta maendeleo na
kumuomba kushugulikia changamoto alizozitoa kwa wananchi ili kuendelea
kujijengea imani kwa wananchi wa kata hiyo.
Mtove aliongeza kuwa
atahakikisha kata yake inamaliza tatizo la maji ambao limetumu kwa miaka mingi
hivyo wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa kujituma ili kukuza uchumi wa kata
hiyo.
“Angalia hadi saizi
tumechimba visima zaidi ya sita kwenye kata yangu japo bado sana kumaliza
tatizo hili la maji hivyo naendelea kujituma kutafuta marafiki,wafadhili na
kumshirikisha mbunge Kabati kusaidia kutatua tatizo la maji na changamoto
nyingi ili wananchi wangu wafanye kazi kwa kujituma bila kuwa na vikwazo
vyovyote vile vya kiafya”.alisema Mtove.
No comments:
Post a Comment