Mratibu wa Mafunzo
ya Mabingwa wa Tiba ya Mifupa nchini (SICOT , Société
Internationale de Chirurgie Orthopédique et de Traumatologie) Dk. Robert Mhina (kulia) kutoka Taasisi ya Mifupa
Tanzania (MOI) , akishiriki mafunzo ya utoaji huduma kwa majeruhiwa wa ajali
kwa njia ya video yaliyoratibiwa na kufanyika kwa njia ya video kwenye kumbi za
Wakala ya Mafunzoa kwa Njia ya Mtandao, yakijumuisha nchi. Kushoto ni
Dk.Lukwinyo na Dk.Mbaruku Mlinga.

Madaktari
mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini.
mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini.
Madaktari wa Tiba
ya Mifupa wakishiriki mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Dk.Hamid Masoud,
Dk.Valentine Restus na Dk. Joseph Msemwa.
ya Mifupa wakishiriki mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Dk.Hamid Masoud,
Dk.Valentine Restus na Dk. Joseph Msemwa.
Na Dotto Mwaibale
UMOJA
wa Madaktari Bingwa wa Mifupa Duniani (SICOT) ikishirikiana na Wakala
ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), umetoa elimu ya kutoa huduma
kwa majeruhi wa ajali kwa njia ya mtandao wa mafunzo kwa njia ya video.
Umoja
huo ulitoa elimu hiyo kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa na wataalamu
wa Mifupa kutoka nchi za Tanzania, Marekani, Pakistani na Brazil.
Akizungumza
mara baada ya mafunzo hayo akiwa TaGLA, Dar es Salaam, Mratibu wa Umoja
huo hapa nchini, Dk. Robert Mhina alisema kupitia mafunzo haya wameweza
kujadili mambo mbalimbali yahusuyo ajali za barabarani.
“Huwa
tunajadili mada mbalimbali kama ajali za barabarani kwa kubadilishana
uzoefu na Madaktari wa nchi nyingine kwa kutumia mtandao wa mafunzo kwa
njia ya video, na wakati wote huwa tunazungumza na nchi kutoka mabara
mengine ili kubadilishana uzoefu,”alisema.
Alisema
madaktari hao huwa wanakubaliana katika kujadili mada na kujadili
kuhusu mambo muhimu yanayohusu tiba ya mifupa huku wakipeana majukumu.
“Kupitia
vikao hivi hutusaidia sana hata kwa wale wanafunzi wanaojifunza Ubingwa
kuona kitu gani kinaendelea duniani, bila gharama za kusafiri nje ya
nchi” alisema Dk Mhina.
Alisema
tayari Umoja huu inaangalia uwezekano wa kutoa nafasi kwa wanafunzi
kutembela vituo kingine katika nchi hizo ili kuona na kuongeza uzoefu
zaidi.
“Mwaka
huu kuna vikao kama sita hivi, kikao hiki ni mwazo tu,”alisema na
kuongeza kuwa kupitia mkutano huo itawasaidia wananchi kwa kuboreshewa
ufanyaji wa tiba sahihi za mifupa hivyo kupata huduma za matibabu
zilizoboreshwa kutokana na ajali za barabarani.
Watoa
mada katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video walikuwa ni
pamoja na Dk. Syed M. Avais wa King Edward Medical University, Dk.
Robert D. Zura wa Louisiana State University Health Science Center na
Dk. Robert I. Mhina, wa Taasisi ya Mifupa Tanzania (MOI) kutoka nchini
Tanzania.
No comments:
Post a Comment