Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa
wa Mwanza (Tanroads) Eng. Marwa Rubirya (wa pili kushoto) akizungumza na
wawakilishi wa vikundi vya wanawake wanaoshiriki mafunzo ya ukarabati
na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi,
Jijini Mwanza.
Mratibu Kitengo cha ushirikishaji
wa wanawake katika kazi za barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Ujenzi) Eng. Rehema Myeya (wa pili kulia) akifafanua jambo
kwa washiriki wa mafunzo ya ukarabati na matengenezo ya barabara kwa
kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi, Jijini Mwanza kushoto ni Eng.
Liberata Alphonce kutoka sekta ya ujenzi na wapili kushoto ni Meneja wa
Tanroads mkoa wa Mwanza Eng. Marwa Rubirya.
Eng. Liberata Alphonce kutoka
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sekta ya (Ujenzi) wa pili
kulia akitoa maelezo kwa washiriki wa mafunzo ya ukarabati na
matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi,
Jijini Mwanza.
Mkufunzi wa mafunzo ya kutumia
teknolojia stahiki ya nguvu kazi kutoka Chuo cha Teknolojia stahiki ya
nguvu kazi Mbeya (ATTI) Eng. Richard Kansimba akifafanua jambo kwa
washiriki wa mafunzo ya ukarabati na matengenezo ya barabara kwa kutumia
teknolojia stahiki ya nguvu kazi, Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya
ukarabati na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya
nguvu kazi akichangia mada juu ya teknolojia hiyo.
Washiriki wa mafunzo ya ukarabati
na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi
wakifuatilia mada hiyo Jijini Mwanza.
………………………………………
Serikali imesema itaendelea
kuwajengea uwezo wanawake ili kuweza kushiriki katika shughuli za
matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya barabara kwa kutumia
teknolojia stahiki ya nguvu kazi.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Wakala
wa Barabara Mkoa wa Mwanza (Tanroads) Eng. Marwa Rubirya wakati
akifungua mafunzo ya kozi kwa wanawake wa vikundi vya mikoa ya
Kanda ya
ziwa jijini Mwanza.
“Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano sekta ya (Ujenzi) imekuwa ikitekekeza sera mbalimbali
ikiwemo shughuli za matengenezo yenye kuongeza ushiriki wa wanawake
katika kazi za barabara ili waweze kujikwamua kiuchumi”. amesema
Eng.Rubirya.
Eng. Rubirya amewataka wanawake
kusijili vikundi vyao kupitia bodi ya usajilibwa Makandarasi nchini
(CRB) ili zabuni za kazi za ukaraba na matengenezo ya barabara
zinapotangazwa waweze kukidhi vigezo vya kupata kazi hizo.
Aidha, Eng. Rubirya amewahimiza
wakinamama hao kufanya kazi hizo kwa ubora unaotakiwa pindi wapatapo
kazi hizo ili barabara hizo ziweze kudumu kwa muda mrefu na kuleta faida
kwa wananchi.
Naye muwezeshaji katika mafunzo
hayo Eng. Liberata Alphonce amesema Serikali imelenga kuinua uchumi wa
wanawake wenye nia ya kufanya kazi za barabara kwa vile uchumi wa
mwanamke ukiimarika na taifa pia litaimarika.
“Kwa muda mrefu kazi za barabara
zimekuwa zikionekana za kiume sasa umefika wakati wa wanawake kushiriki
katika kazi hizo kwa vile uwezo tunao.” amesisitiza Eng.Alphonce.
Kwa upande wake Mratibu wa kitengo
cha ushirikishaji wanawake katika kazi za barabara Eng. Rehema Myeya
amesema Wizara imeona umuhimu wa kutoa mafunzo yatakayowasaidia wanawake
kuwa na uwezo wa kufanya kazi za ukandarasi hasa wa barabara hususan
matengenezo na ukarabati.
“Tumekuwa tukitoa mafunzo haya kwa
wanawake katika sehemu mbalimbali nchini na sasa tupo Mwanza lengo ni
kuwafundisha namna ya kufanya kazi hizi za ukandarasi kwa weledi
unaotakiwa”. amesema Eng.Myeya.
Teknolojia stahiki ya nguvu kazi
inahusisha utumiaji wa rasilimali zilizopo pamoja na kutumia vitendea
kazi rahisi na mitambo midogo midogo midogo katika ujenzi na ukarabati
wa barabara.
Imetolewa na Kitengo cha habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment