Na: Frank Shija – MAELEZO
FEMINA Hip yatoa tuzo tano za mwaka kwa Klabu za Fema ambazo zimefanya vizuri katika Nyanja mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Femina Hip Dkt. Minou
Fuglesang wakati wa Kongamano la mwaka la Vijana leo jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa tuzo
hizo zinatolewa ili kutia chachu kwa vijana kuongeza bidi katika
kutatua changamoto zao kwa kujiamnini huku wakiwa na ujuzi mwepesi
utakaowaomgezea umakini katika shughuli zao.
“Tmezigawa tuzo hizi katika makundi makuu matano ambayo ni Mtandao Bora wa Klabu ya Fema ambayo imekwenda kwa Mwanza Federation Fema Clubs, Mshindi wa Pili wa Mtandao Bora wa Klabu za Fema iliyochukuliwa na Dodoma Students and Teachers”.Alisema Fuhlesang.
Tuzo zingine kuwa ni Mhamasishaji
Bora wa Mtandao wa Klabu za Fema wa mwaka iliyokwenda kwa Mwalimu
Christopher Mavunde, Mhamasishaji Bora wa Klabu za Fema wa mwaka
iliyochukuliwa na Mwalimu Bryson Paul kutoka Ngweli FEMA Klabu – Shule
ya Sekondari Ngweli wilayani Sengerema pamoja na Klabu bora ya FEMA kwa
mwaka ambayo ni Kisihigh Fema Club kutoka Shule ya Sekondari Kisimiri
mkoani Arusha.
Akizungumza katika mkutano huo
Mkurugenzi huyo amesema kuwa FEMINA Hip imekuwa ikiendesha program za
kuwakutanisha vijana ili kuwajengea uwezo katika Nyanja za mabalimabali
ikiwemo uongozi kwa manufaa ya sasa na baadae.
Ujuzi ambapo vijana wamekuwa
wakipatiwa kutoka kwa wataalamu wa Shirika hilo ni pamoja na
mawasiliano,mabadiliko ya mitazamo,elimu juu ya afya ya uzazi, malezi na
makuzi pamoja na stadi za maisha.
Kwa upande wake mshindi wa tuzo
Mhamasishaji Bora wa Klabu za Fema wa mwaka 2017 Mwalimu Bryson Paul
amesema kuwa Klabu za FEMA zimekuwa msingi imara wa kuwajengea uwezo wa
kujitambua vijana wengi nchini hivyo ni vyema watanzania wakatambua
umuhimu wa vijana wao kushiriki katika vikundi hivyo ambavyo vimekuwa na
lengo la kuwajengea uwezo kwa kuwapa elimu na ujuzi mbalimbali ikiwemo
stadi za maisha.
Aliongeza kuwa binafsi
amefarijika kwa kuibuka kuwa mshindi katika kipengele hicho na
kusisitiza kuwa siri pekee ni nidhamu na moyo wa kujifunza Zaidi kwa
kushirikiana na wenzako.
FEMINA Hip imewakutanisha vijana
walikatika Klabu za FEMA kutoka pande zote za nchi katika Kongamono
lililofanyika katika hoteli ya Belinda Jijini Dar es Salaam, ambalo
pamoja na utoaji wa tuzo pia vijana walipata fursa ya kujadiliana mambo
mbalimbali kuhusu elimu na masuala mtambuka kwa vijana.
No comments:
Post a Comment