Collins Saliboko akijaindaa ‘ku-dive’ au kuchupa katika bwawa la Chuo cha St Felix, Uingereza)
Muogeleaji wa Tanzania, Celina Itatiro akichupa kwenye mashindano ya Afrika Kusini
Collins Saliboko akichapa maji St Felix College, Uingereza.
Celina Itatiro (Mwenye kofia ya orange) akiogelea huku akiwa na glasi ya maji kwenye paji la uso.
Collins Saliboko (wa kwanza
kulia) akiwa na waogeleaji wa Tanzania wanao soma St Felix College;
Aliasgar Karimjee na Sonia Tumiotto mara baada ya kutwa medali katika
mashindano ya chuo.
Na Mwandishi wetu
Muogeleaji
chipukizi wa Tanzania, Collins Saliboko ambaye ataiwakilisha Tanzania
katika mashindano ya Jumuiya ya Madola ya Vijana ameahidi kuipeperusha vyema na kuiweka histori katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza.
Mbali
ya Collins ambaye anashindana kwa upande wa wanaume, msichana, Celina
Itatiro ataiwakilisha nchi kwa upande wa wanawake katika mashindano hayo
yaliyopangwa kufanyika nchini Bahamas kuanzia Julai 18 mpaka 23 kenye
mji wa Nassau.
Collins
ambaye kwa sasa anasoma Chuo cha St Felix, Uingereza, amesema kuwa
ameanza mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo chini ya kocha wake, Sue
Purchase amesema kuwa amepania kufanya kile ambacho watanzania wengi
hawatakitarajia kupitia mchezo wa kuogelea ambao kwa sasa unakuja juu
kwa kasi.
Alisema
kuwa atatumia pia mazoezi ya timu ya kuogelea ya chuo chao kama sehemu
ya maandalizi, kabla ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ambayo
itatangazwa hapo baadaye.
“Naahidi
kuitendea haki nafasi hii, hii inatokana na juhudi zangu katika mchezo
wa kuogelea, matokeo yangu bora ndiyo yamenipa nafasi hii, naona mwanga
katika mchezo wa kuogelea na ninaahidi kufanya vyema,”
“Mazoezi
ya hapa St Felix ni mazuri sana, hii inatokana na vifaa bora na walimu
wazuri, hapa ia kuna ushindani mkubwa na hivi juzi juzi
tu nilishinda nafasi ya pili kwenye mashindano ya huku Uingereza, ni
matokeo mazuri na ninaahdi kufanya vyema zaidi,” alisema Collins kwa
njia ya simu.
Alisema
kuwa mpaka sasa ameshiriki katika mashindano mengi ya ngazi ya chuo na
kupata matokeo mazuri. “Mashidano haya ya Chuo ni sehemu ya maandalizi
yangu, naishi hapa chuoni, kila Napata muda mwingi wa kujifunza, Mwalimu
wangu, Sue ni mkali na kwa sasa anajua jukumu langu la kitaifa,
ameongeza ‘dozi’ ya mazoezi,” alisema.
Katibu
Mku wa Chama Cha kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhan Namkoveka alisema
kuwa kazi iliyopo sasa ni kwa makocha kuwaandaa wachezaji katika matukio
watakaoshiriki ili kuweza kufanya vizuri.
Namkoveka
alisema kuwa mbali ya kusaka medali, lengo kuu la chama kwa wachezaji
hao ni kupunguza muda wao ili baadae waweze kufikia muda unaotakiwa na Shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani, (FINA) kiwango cha muda B au A.
Mashindano ya jumuiya ya madola haya yatakuwa ya sita baada ya kuanzishwa kwake mwaka 2000 na wakitegemewa vijana 1000 wenye umri wa miaka kuazia maika 14 hadi 18 kushindana katika michezo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment