Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa
Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akikinga maji
kwenye ndoo kuashiria sasa kisima cha maji kimefunguliwa na kuanza
kutumia kwa wakazi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa akiwa na
diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa
Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akisikiliza
maelezo kutoka kwa mtaalam wa kujimba visima ambaye pia ndiye
aliyechimba kisima hicho.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa
Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji
waliyokuwa wanatumia wananchi mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa.
Na haya ndio maji waliyokuwa wanatumia wananchiwa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa kabla ya kujimbiwa kisima
…………………………………………………………………….
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wananchi wa mtaa wa Igungandembwe
manispaa ya Iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa
Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na diwani wa
kata ya
Nduli Bashir Mtove kwa msaada wa kuwachimbia kisima cha maji safi na
salama.
Wakizungumza na blog hii wananchi
hao wamesema kuwa wanatakribani miaka hamsini na tatu (53) hawajawahi
pata maji masafi na salama.
“Angalia maji haya machafu ndio
tulikuwa tunakunywa na kupikia ila mungu alikuwa anatusaidia tu
kutuepusha na magonjwa mbalimbali kiukweli leo tunafuraha sana kuanza
kutumia haya maji na ndio maana unaona wananchi wanafuraha nawameanza
kunywa maji hapa hapa kwenye kisima hiki kwa kuwa bado hawaamini
kilichotokea”,walisema wananchi.
Wananchi wao wamemuomba mbunge
Ritta kabati na Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove kuendelea kutatua
changamoto za wananchi kwa kuwa walichaguliwa na wananchi kwa lengo la
kuwatumikia.
Kwa upande wake mbunge wa viti
maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
alisema kuwa wataendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa
kuwa yeye ni mbunge wa wananchi wote bila kubagua vyama.
Kabati alisema kuwa ataendelea
kuwachimbia visima na kukarabati majengo ya shule zilizochakaa katika
mkoa wa Iringa kwa kuwa yeye ni mbunge wa mkoa wa Iringa hivyo aliwaomba
wananchi kuendelea kuiamini serikali ya chama cha mapinduzi kwa kazi
kubwa wanayoifanya kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr John Pombe Magufuli.
“Hivi hamuoni nimeamua kufika
huku ambako hata viongozi wengi hawajafika ila mimi nimekuja nimewaleta
kisima na maji safi na nitaendelea kuja kutatua matatizo ya mtaa huu kwa
kuwa tumetumwa na Rais kufanya kazi kwa wananchi wa chini ndio maana
hata mimi nimeanza kufanya kazi huku mbali japo kuwa ndio jadi yangu
kuwatumikia sana wananchi wa chini sasa naombeni mniunge mkono katika
juhudi zangu za kuwaletea mandeleo”.alisema Kabati
Aidha Kabati alisema kuwa lengo
la serikali ya awamu ya tano ni kuleta maendeleo kuanzia huku chini
kupanda juu hivyo tufanye kazi kwa kujituma ili tuende sambamba na kasi
ya Rais wetu.
Naye Diwani wa kata ya nduli
Bashir Mtove alimshukuru mbunge huyo kwa jihada zake za kuleta maendeleo
na kumuomba kushugulikia changamoto alizozitoa kwa wananchi ili
kuendelea kujijengea imani kwa wananchi wa kata hiyo.
Mtove aliongeza kuwa atahakikisha
kata yake inamaliza tatizo la maji ambao limetumu kwa miaka mingi hivyo
wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa kujituma ili kukuza uchumi wa kata
hiyo.
“Angalia hadi saizi tumechimba
visima zaidi ya sita kwenye kata yangu japo bado sana kumaliza tatizo
hili la maji hivyo naendelea kujituma kutafuta marafiki,wafadhili na
kumshirikisha mbunge Kabati kusaidia kutatua tatizo la maji na
changamoto nyingi ili wananchi wangu wafanye kazi kwa kujituma bila kuwa
na vikwazo vyovyote vile vya kiafya”.alisema Mtove.
No comments:
Post a Comment