Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifungua kikao cha Wadau wa Elimu Mkoa wa Arusha
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akishirikiana na wataalamu kuweka
mitambo sawa kwa ajili ya wadau wa Elimu kuwasilisha taarifa.
Viongozi wa Halmashauri ya Ngorongoro wakifuatilia Kikao cha Wadau wa Elimu
Wadau wa Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
Kaimu
Afisa Elimu Mkoa Emmanuel Mahondo akiwasilisha taarifa ya Elimu Mkoa
wakati wa Kikao cha wadau wa Elimu kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu
wa Mkoa wa Arusha.
…………………………………………………………………………
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo amewataka wadau wa elimu kuunganisha nguvu zao
katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ili kufikia malengo
ya Serikali ya ufaulu wa asilimia 80 kila wilaya.
Gambo ametoa wito huo katika
kikao chake na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri ,Maafisa
Elimu wa Shule za Sekondari na Msingi pamoja na wadau wengine wa Elimu
mkoani hapa.
Alisema ili kufikia malengo ya
Matokeo Makubwa Sasa(BRN) yanayotaka ufaulu katika ngazi ya Elimu ya
Msingi na Sekondari kufikia asilimia 80 lazima kuwepo na vifaa
vinavyohusika kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia.
“Katika kuangalia elimu kwa
mapana yake, hatuna budi kuwajengea uwezo walimu wetu kwa kuwapa mafunzo
ya mara kwa mara ili kuwapa motisha badala ya kuwaacha na elimu
waliyoipata Chuoni pekee,” alisema Gambo
Pia aliagiza Halmashauri zote za
Mkoa huu kununua Mashine za kufyatulia matofali tambazo zinapatikana kwa
gharama nafuu kutoka shirika la viwanda vidogo (Sido) ili kurahisisha
zoezi la ufyatuaji wa matofali kwa matumizi ya Shule.
Aliwataka Wakuu wa Wilaya Mkoani
hapa kuona namna wanavyoweza kuwashirikisha wananchi kuchangia nguvu zao
katika kufyatua matofali mara baada ya halmashauri kukamilisha ununuzi
wa mashine za kufanyia kazi hiyo toka Sido.
“Uchakavu wa majengo na upungufu
wa vyumba vya madarasa pamoja na vyoo imekua ni changamoto ya muda mrefu
katika Sekta ya Elimu lakini viongozi mkifanikiwa kuwahamasisha
wananchi kuchangia nguvu kazi katika miradi ya Elimu itasaidia
kukarabati na kukamilisha ujenzi wa miundombinu kwa wakati muafaka hivyo
kuboresha upatikanaji wa Elimu bora kwa watoto wetu”.
Naye kaimu Afisa Elimu mkoa wa
Arusha, Emmanuel Mahondo amesema hali ya elimu imekua ikiimarika kwa
ufaulu kuongezeka na kuwa katika mkoa wa Arusha ni halmashauri za Arusha
Jiji na Arusha DC ndizo zilifikia viwango BRN.
Kikao hiki na wadau wa Elimu ni
muendelezo wa vikao vya Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na wadau wa sekta
mbalimbali katika Mkoa huu kujadili changamoto na kuona namna ya
kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja.
No comments:
Post a Comment