MKUU WA MKOA WA LINDI APIGA MARUFUKU MATUMIZI MABAYA YA CHAKULA KWENYE SHEREHE ZA KIMILA
Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa anaongea na wanakijiji wa Kijiji cha Makanjiro
Mkuu Wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na wananchi wa kijiji cha Mandawa(Na: Mwanakheri Ahmed wa Ruvumatv.com)
…………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mhe.Godfrey Zambi amepiga marufuku kufanyika kwa shughuli zozote zile za kimila zinazotumia chakula kuanzia mwezi wahuu wa Disemba mpaka Mei 2017.
Shughuli hizonipamoja naUnyago, NdoanaNgoma za Majini.Alisema shughuli hizo zinazofanywa naWananchi zimekuwa zinatumia chakula kingi hali hii inaweza kupelekea kutokea kwa janga lanjaamkoani hapo.
Mkuu huyo waMkoawa LindialiwatakaWananchi kuwa wavumilivu na waelewa kwani janga la njaa halichaguiMkoa bali matumizi mabovu ya chakula yanaweza kuleta janga hilokwa Wananchi wote.
“Sitaki kuwaMkuu wa Mkoa ambaye Mkoa wanguumekutwa na janga la njaa kwani hii ni aibu kubwa hivyoWatu wawe makini katika matumizi ya chakula hata kama chakula wanalima kwa nguvu zao wenyewe“.
Wakati huo huo Mhe. ZambialiwatakaWananchi wa
Ruangwa wajenge vyoo imara na vya matumizi ya muda mrefu, ili kuweza
kujiepusha na maradhi ya Kipindupindu kama ambavyo yanaikabili Wilaya ya
Kilwa.
Aidha, Mkuu wa Mkoa aliwataka Watendaji wa vijiji kusimamia zoezi la kila Mwananchi wa eneo lake anakuwa na choo imara naMtu atakaekaidi kufanya ujenzi wa choo cha nyumbani kwake basi achukuliwe hatua za kisheria.
Vilevilealiwasa
Wananchi kuwa na matumizi mazuri ya pesa wanazoipata za kuuza korosho
au fidia wanazolipwa na kuacha matumizi mabovu ya pesa hizo kama ambaVyo
inafanywa na baadhi yaWatu.
Mhe.Zambi aliwakata Wananchi kutumia pesa wanazozipata katika kutengeneza maisha yao kama katika kusomeshaVijana wao na kujenga nyumba imara kwa ajili ya familia zao.
No comments:
Post a Comment