Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania leo, Mjini Dodoma limepisha Muswada wa Sheria ya Huduma ya
Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).
Waziri wa Mambo ya Katiba na
Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akitoa taarifa wakati wa
kuwasilisha muswada huo amesema kuwa muswada huo wa sheria umepitia
hatua
nyingi na umechukua muda mrefu hadi kufikia hatua ya kujadiliwa na
Bunge tukufu.
Aliendelea kwa kusema kuwa
muswada huo unapendekeza kutungwa kwa sheria ya msaada wa kisheria kwa
lengo la kuanzisha (kwa mara ya kwanza katika histori ya nchi) mfumo wa
kisheria wa kusimamia, kuratibu, kurasimisha na kutambua utoaji wa
huduma ya msaada wa kisheria katika mashauri yote ya Jinai na Madai kwa
mahitaji.
Aidha utaratibu uliokuwepo kwa
miaka mingi kwa upande wa Serikali unahusu baadhi tu ya makosa ya Jina,
makosa yenye adhabu kubwa kama vile ya kunyongwa hadi kufa na vifungo
virefu. Ambapo huduma hiyo imekuwa ikitolewa katika ngazi ya Mahakama
Kuu pekee na kwa wigo mdogo tu pale inapohitajika kwa maslahi ya haki na
kwa maelekezo ya Jaji Mkuu au yeyote aliyekasimiwa mamlaka ya kutoa
maelekezo hayo.
“Kumekuwepo na ongezeko kubwa la
mahitaji ya huduma ya msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria.
Kutokana na hali hiyo, Serikali imeona ulazima wa kuanzisha mfumo wa
kusimamia na kuratibu utoaji wa huduma hiyo ili kuhakikisha inatolewa na
watu wenye sifa, kwa wahitaji halisi na kwa taratibu zinazofahamika ili
iendane na matakwa ya kikatiba,” alifafanua Dkt. Mwakyembe.
Vile vile ameeleza kuwa muswada
huo unalenga kuwatambua wasaidizi wa kisheria, kufuta sheria ya msaada
wa kisheria (katika mashauri ya Jinai).
Kwa upande wake Mbunge Selemani
Zedi amesema kuwa, muswada huo utawasaidia wananchi ambao hawana uwezo
wa kuwalipa Mawakili wanapohitaji msaada wa Kisheria.
Aidha, Naibu Spika Dkt. Tulia
Ackson ameipongeza Serikali kwa muswada huo muhimu ambao Bunge
umeipitisha unasuobiria kutiwa saini na Mhe. Rais ili kuwa Sheria.
No comments:
Post a Comment