Waziri wa Maliasili na Utalii,
Prof. Jumanne Maghembe wa pili kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa kwanza kulia)
wakiwa kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini
mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili nchini tangu
novemba 2015 hadi novemba 2016, uliowakutanisha wadau wa Maliasili
kutoka sekta binafsi na Serikalini kujadili sekta za misitu ,
wanyampori pamoja na mambo kale.
Baadhi ya wadau wa Maliasili
kutoka serikalini na Sekta binafsi wakifuatilia kwa makini uwasilishaji
wa mada za Maliasili kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam wa kutathmini mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya
maliasili nchini tangu novemba 2015 hadi novemba 2016. ( Picha na
Lusungu Helela- Maliasili)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Eng. Angelina Madete akichangia hoja kwenye
mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa kutathmini mafanikio na
changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili nchini tangu novemba 2015
hadi novemba 2016. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Prof. Jumanne Maghembe wa akiwa na wadau wa Maliasili wakisiliza kwa
makini uwasilishaji wa mada kuhusu sekta za misitu , wanyampori pamoja
na mambo kale kwenye mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam wa
kutathmini mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili
nchini tangu novemba 2015 hadi novemba 2016.
Picha na Lusungu Helela- Maliasili.
…………………………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Prof. Jumanne Maghembe amesema Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa
hakuna magogo na malighafi ya misitu yatakayosafirishwa kwenda nje ya
nchi kabla ya kuchakatwa.
Amesema , hiyo itasaidia kuongeza
thamani pamoja na kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wengi kwa
kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kutengezea vifaa
mbalilmbali vitakanavyo na mazao ya misitu kutokana na Magogo na
Malighafi ya misitu kuchakatwa ndani ya nchi.
Amesema hayo leo kwenye mkutano wa
kutathmini mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili
nchini tangu novemba 2015 hadi novemba 2016, uliowakutanisha wadau wa
Maliasili kutoka sekta binafsi na Serikalini kujadili sekta za misitu ,
wanyampori pamoja na mambo kale
Amesema kuwa Misitu ni sekta
inayokabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukataji miti hovyo uvunaji
haramu wa magogo pamoja na usafirishaji haramu wa magogo kwenda nje ya
nchi.
Amesema katika kukabiliana na
changamoto hizo Serikali imeanza kuona namna ya kuwalipa sekta binafsi
na watu wenye kipato cha chini cha kati watakaokuwa wanapanda miti
kama motisha kutokana na mchango mkubwa wa misitu wa kuzalisha hewa
safi duniani kwa kuondoa hewa ya ukaa.
Amesema mpango huo kamambe wa
kuwalipa watakaopanda miti kwa wingi itakuwa ni njia muafaka ya
kuondokana na tatizo la ukame linaaloendelea kutokea kutokana miti mingi
kuendelea kukatwa kwa ajili ya mkaa na matumizi mengine kuongezeka kwa
kasi.
No comments:
Post a Comment