Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Agnes Mtawa akizungumza na wauguzi baada ya wauguzi hao kutoa zawadi
kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo. Zawadi hizo zimepokelewa
na mtoto Neema Selemani kwa niaba ya wagonjwa wengine. Kutoka Kushoto ni
Mkuu wa Jengo la watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja na Katibu wa Tughe Tawi La Muhimbili, Bw. Faustine Fidelis.
Baadhi ya wauguzi wakiwa katika hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wagonjwa mbalimbali.
Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Bi. Agnes Mtawa akitoa zawadi kwa mtoto Neema Selemani ambaye amepokea
kwa niaba ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.
Wauguzi wakifuatilia hafla hiyo leo.
Mkuu wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja (katikati) akiwa amevishwa kitenge baada ya kupewa zawadi na wauguzi wenzake.
Meneja
kutoka majengo mbalimbali katika hospitali hiyo wakiwa katika hafla
hiyo Leo. Kutoka Kulia ni Meneja wa Jengo la Ufuaji, Bi. Lina Kinabo,
Meneja wa Jengo la Upasuaji, Bi. Jane Chuwa, Meneja wa Jengo la Huduma
za Nje, Bi. Juni Samwel na Meneja wa Jengo la Sewahaji, Bi. Salome
Mayenga.
Mkuu
wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja akimkabidhi Mkurugenzi wa
Uuguzi katika hospitali hiyo, Bi. Agnes Mtawa zawadi maalamu.
Bi. Anna Mponeja akimlisha keki mtoto Neema Seleman Leo katika hospitali hiyo.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
…….
Baadhi
ya wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), leo wametoa zawadi
mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.
Akizungumza
katika hafla hiyo fupi, Mkurugenzi wa Uuguzi katika hospitali hiyo, Bi.
Agnes Mtawa amewashukuru wauguzi hao kwa kuonyesha ushirikiano katika
kazi na kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa.
Mtawa
aliwaasa wauguzi kuendelea na upendo huo waliouonyesha katika kipindi
chote cha mwaka 2016 kwa kuwa ndio upendo ambao Mungu anataka wauonyeshe
kwa wagonjwa.
Pia,
aliwapongeza kwa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika mwaka huu
na kuwataka kutumia changamoto hizo kama sehemu ya mikakati ya mwaka
2017.
Naye
Meneja wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja aliwashukuru
wauguzi kwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa katika kipindi chote cha
mwaka 2016.
Hafla hiyo imeudhuriwa na zaidi ya wauguzi 70.
No comments:
Post a Comment