Mwakilishi
Mkazi wa Taasisi ya Sura Mpya na Sauti Mpya Tanzania (NFNV), Emma
Kawawa (kulia), akizungumza na wanawake wafanyabiashara katika masoko ya
Ilala na Temeke wakati akifunga mkutano wa kupanga na kuweka mikakati
ya vikundi vya umoja na umoja wa kitaifa wa wanawake (Uwawasota) kwa
mwaka 2017 uliofanyika Hoteli ya Dreamer Buguruni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele (kulia), akizungumza katika ufungaji wa mkutano huo.
Ofisa Mradi na Mwanasheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mussa Mlawa (kushoto), akiteta jambo na Ofisa Uwezeshaji Jamii Kiuchumi wa Shirika hilo, Theresia Jeremia .
Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye mkutano huo.
Ofisa Mradi na
Mwanasheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mussa Mlawa
(kulia), Mwezeshaji sheria masokoni, Consolatha Cleophas na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele wakifuatia kwa karibu mafunzo hayo.
Mwezeshaji
wa sheria katika Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa akiandika
changamoto na za uendeshaji na usimamizi wa umoja kwenye masoko.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Makofi yakipigwa baada ya hutuba ya mgeni rasmi Emma Kawawa.
Usikivu katika mkutano huo.
Mafunzo yakiendelea,
Mgeni rasmi Emma Kawawa akifunga mafunzo hayo.
Tabasamu wakati wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha hiyo
Na Dotto Mwaibale
WANAWAKE
Wajasiriamali nchini wametakiwa kuwa na mshikamano, uthubutu, na upendo
ili kusonga mbele katika shughuli zao za kiuchumi.
Mwito huo
ulitolewa na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Sura Mpya na Sauti Mpya
Tanzania (NFNV), Emma Kawawa ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifunga
mkutano wa kupanga na kuweka mikakati ya vikundi vya umoja na umoja wa
kitaifa wa wanawake (Uwawasota) kwa mwaka 2017 uliofanyika Hoteli ya Dreamer Buguruni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
“Mkitaka
kusonga mbele kiuchumi kupitia ujasiriamali wenu kama wanavyo fanya
wanawake wenzetu katika nchi mbalimbali duniani mnapaswa kuwa na
uthubutu, kupendana, kuacha majungu, kutunza muda na kushirikiana”
alisema Kawawa.
Ofisa
Mradi na Mwanasheria wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Mussa
Mlawa alisema lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha viongozi wa vikundi
vya umoja wa wanawake kwenye masoko ya Manispaa ya Ilala na Temeke ili
kuweza kujadili changamoto za uendeshaji na uimarishaji wa umoja
masokoni kwa mwaka 2017.
“Malengo
mengine ya mkutano huu ni kutengeneza mpango kazi wa kufufua na
kuimarisha umoja masokoni kwa mwaka 2017, kupeana mrejesho wa usajili wa
umoja wa kitaifa (Uwawasota) na kupokea taarifa ya kamati ya
uhamasishaji wa umoja kwa mwaka 2016” alisema Mlawa.
Ofisa
Uwezeshaji Jamii Kiuchumi wa Shirika hilo, Theresia Jeremia alisema
mkutano huo uliwahusisha wanawake wajasiriamali kutoka masoko sita ya
katika manispaa za Temeke na Ilala ambayo ni Gezaulole, Tabata Muslimu,
Ferry, Temeke Sterio na Mchikichini.
No comments:
Post a Comment