Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo,
ambaye pia ni msemaji mkuu wa serikali, Dkt. Hassan Abass, (watatu
kushoto), akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa
Mtandao wa wamiliki wa Blogu Tanzania, (TBN), na mafunzo kwa wana
mtandao hao kwenye ukumbi wa jengo la Jubilee Towers la PSPF jijini Dar
es Salaam, leo Desemba 5, 2016
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MKURUGENZI
wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas, amewaondoa hofu wamiliki na
waendeshaji wa mitandao ya kijamii nchini kupitia Mtandao wa Bloggers Tanzania,
TBN, kuwa hawahusiki na usajili katika sheria mpya ya huduma za vyombo vya
habari.
Dkt.
Abbas ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Tanzania Bloggers
Network-TBN, kwenye ukumbi wa Belmonte ulioko jingo la PSPF, Jubilee Towers
jijini Dar es Salaam leo Desemba 5, 2016.
“Napenda
niliweke wazi swala hili la waandishi kusajiliwa chini ya sheria hii mpya,
ukweli ni kwamba, waendesha mitandao ya kijamii hawatahusika na swala la
kusajiliwa ili afanye kazi hiyo,” alsiema
Aidha
Mkurugenzi huyo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali aliwaeleza wanamtandao
hao kuwa, Utoaji wa Press Card, (Vitambulisho vya uandishi habari), kwa sasa
utazingatia matakwa ya sheria ya sasa ya Huduma za vyombo vya habari lakini
akawaondoa hofu kuwa, kanuni zitaundwa ili kuangalia pengine pawepo na press
card zitakazozingatia madaraja mbalimbali (Categories).
“Ninawashauri
ndugu zangu, mnatakiwa mjenge hoja ni kwanini mpatiwe Press Card, lakini uzoefu
unaonyesha zipo baadhi ya nchi Duniani zinatoa press card kwa bloggers, pengine
na hapa kwetu chini ya kanuni tutakazozitengeneza, tunaweza kutoa press card
kwa bloggers pia.” Alifafanua.
Mkutano
huowa TBN umedhaminiwa na benki ya NMB, PSPF, NHIF, Serengeti Beverarge Limited
na Coca Cola.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan
Abass, amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF leo Desemba 5, 2016.
Dkt.
Abbas ambaye ameteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo, alijaza fomu za
kujiunga na Mfuko huo akisaidiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw.
Abdul Njaidi ofosini kwake jingo la Jubilee Towers barabara ya Ohio jijini Dar
es Salaam.
Mtoa mada Krant Mwantepele
Dkt. Abass, akifurahia jambo na mmiliki wa Michuzi Blog, Bw. Muhidin Issa Michuzi, "Ankal"
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na
Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati
akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar
es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim
Mushi.
Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za
Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili (kulia), akizungumza katika
mkutano huo kuhusu masuala mbalimbali ya benki hiyo ambayo ni moja ya
mdhamini wa mkutano huo.
Mwanahabari na Blogger Frederick Katulanda (kulia), akiuliza swali.
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi (kushoto), akiwaelekeza jambo mablogger
Mablogger wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mablogger kazini
Blogger Baraka kutoka Bukoba akiuliza swali.
Mwezeshaji wa mkutano huo Maxsence Mello akitoa mada.
Meza kuu. Kutoka kulia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Krant Mwantepele.Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili,Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas,
Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi pamoja na Katibu wa muda wa
TNB, Khadija Kalili
Blogger Mroki Mroki akiwa kazini wakati wa mkutano huo.
Mgeni rasmi akihutubia.
Mwendeshaji wa mtandao wa FullShangwe, John Bukuku akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NMB wakibadilishana mawazo. Kushoto ni Doris na Joyce Nsekela.
Blogger kutoka mkoani Arusha, Tumaniel
Seria (kulia), akiuliza swali. Kusho ni William Malecela mmiliki wa
mtandao wa Mwananchi na katikati ni mmiliki wa Blog ya Michuzi Issa
Michuzi.
Mmiliki wa mtandao wa Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda akichangia jambo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment