Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu msaada wa dola za Kimarekani 50,000/= sawa na shilingi milioni
108 za Kitanzania zilizotolewa na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Bw.
Song, Geum-young leo jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetalewa kwa
ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na makazi yaliyoathiriwa na
Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 septemba 2016.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga (kulia) akipokea mfano wa hundi
yenye thamani ya dola za Kimarekani 50,000/= sawa na shilingi milioni
108 za Kitanzania zilizotolewa na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Bw.
Song, Geum-young leo jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetalewa kwa
ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na makazi yaliyoathiriwa na
Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 septemba 2016.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga (kushoto) akiagana na Balozi wa
Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum-young mara baada ya kupokea
msaada wa Dola za Kimarekani 50,000 leo jijini Dar es Salaam. Msaada huo
umetalewa kwa ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na makazi
yaliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9
septemba 2016.
Picha na MAELEZO.
…………..
Na: Frank Shija – MAELEZO.
Tanzania yadhamiria kuimarisha
uhusiano baina yake na Jamhuri ya Korea kwa kufungua Ofisi zake za
Ubalozi Mjini Seoul, nchini Korea.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine
Mahiga leo jijini Dar es Salaam wakati akipokea msaada wa Dola za
Kimarekani 50,000 kwa ajili ya kusaidia urejeshaji wa miundombinu
iliyoharibika kutokana na Tetemeko la Ardhi lilitokea Mkoani Kagera
mnamo tarehe 9 Septemba 2016.
Balozi Mahiga amesema kuwa nchi ya
Jamhuri ya Korea imekuwa na uhusiano mzuri na wa muda mrefu na Tanzania
ambapo kupitia uhusiano huo imekuwa ikisaidia katika mambo mbalimbali
ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya akitolea mfano
Hospitali za Mloganzila na Chanika ambazo zote zimejengwa kwa ufadhili
wa Shirika la Kimataifa la Mahusiano la Korea (KOICA).
“Korea imekuwa na Ofisi za Ubalozi
hapa nchini kwa zaidi ya miaka 25 hivyo wameona ni wakati sasa kwa
Tanzania kuwa na Ofisi yake Ubalozi nchini nnchini Korea,” Alisema
Balozi Mahiga.
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri
ya Korea nchini Bw. Song, Geum – Young amesema kuwa msaada huo unatokana
na namna ambavyo waliguswa na janga la Tetemeko la ardhi lililotokea
Mkoani Kagera na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na makazi
ya wananchi.
Ameongeza kuwa msaada huo ni
sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa Rais Dkt. Magufuli
alipomtembelea Ikulu na kumpa Pole mnamo tarehe 22 Septemba mwaka huu.
Balozi Song Geum-Young pia
amemhakikishia Waziri Mahiga kuwa Korea itaendeleza na kuimarisha
uhusiano wake na Tanzania na kwamba itatoa ushirikiano wa kutosha
kufanikisha miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa hapa nchini ikiwemo
ujenzi wa Daraja la Salender, Meli, Hospitali ya Mloganzila, Chanika na
mingineyo.
No comments:
Post a Comment