Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimkabidhi zawadi ya dawa
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.
Mohamed Janabi ambazo zitatumika kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Prof. Ayoub Magimba na Kulia
ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge. (PICHANA ANNA NKINDA WA JKCI)
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akisaini kitabu cha wageni alipotembelea
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam ili kuona ni
jinsi gani nchi yake itakavyoisaidia Taasisi hiyo. Kulia kwa Balozi ni
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi.
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati balozi
huyo alipotembelea Taasisi hiyo na kuahidi kuisaidia vifaa vya kutunzia damu na
kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji wa moyo katika chumba cha upasuaji. Kulia
ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge.
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya gari na ndege ya kuchezea
Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo huku Mama yake Jumanne akishuhudia.
Daktari
Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Peter
Kisenge akimuelezea takwimu za upasuaji wa wagonjwa wa Moyo zinazofanywa na
Taasisi hiyo Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem (kushoto). Wapili
kulia ni Dkt. Barjces Almutairi kutoka Mfuko wa Kusaidia wagonjwa wa nchini
Kuwait akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo Tulizo Shemu Sanga.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akiongea jambo na Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem wakati balozi
huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam ili kuona namna
gani nchi yake inaweza kusaidia vifaa tiba.
Balozi
wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Ubalozi wa Kuwait mara
baada ya kumalizika kwa ziara yake aliyoifanya katika Taasisi hiyo. Kulia kwa
Mhe. Balozi ni Mkurugenzi Mtendaji JKCI Prof. Mohamed Janabi
No comments:
Post a Comment