Wakati
wanachuo wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha mjini Mbeya
wakiahidi kupeleka vijijini kampeni ya malengo ya maendeleo endelevu
(SDGs) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amesema
kwamba utekelezaji wa malengo hayo uko mikononi mwa vijana zaidi.
Alisema nchini Tanzania zaidi ya nusu ya watu wake ni vijana hivyo
wakielewa malengo hayo itakuwa rahisi kushawishi wengine kuhuisha
maendeleo hayo na shughuli zao za kila siku huku wakitunza mazingira.
Alisema shauri kwanini malengo yamekuwa mengi wakati yale ya Milenia
yalikuwa nane tu, Mratibu huyo alisema kwamba suala si uwingi wa malengo
bali maana yake na haja ya utekelezaji.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel
Mosses akimkaribisha na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
aliyemtembelea ofisini kwake mjini Mbeya.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Alisema
MDGs (Malengo ya Millennia) iliacha masuala kadhaa bila uelekeo ikiwamo
suala la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuwapo kwake
kunahakikisha uwapo wa maendeleo endelevu kwa kuwa kila kitu kinategemea
sana mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa. Alisema ni matumaini yake
kwamba kuzinduka kwa jamii ya vijana itasaidia kukabiliana na changamoto
hizo za sasa za dunia. Kauli ya mratibu huyo iliungwa mkono na wanachuo
hao ambao walisema kwamba wanaona uhalisia wa mahitajhi ya sasa na
kwamba watawasilisha kampeni hiyo maeneo wanayotoka ili kuwapo na
mabadiliko.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel
Mosses akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez aliyeambatana na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa
Mataifa nchini, Hoyce Temu.
Kwa
kuwa wengi ni vijana na kwa kuwa asilimia 75 ya vijana wanaishi
vijijini, itakuwa heri kama walivyofundishwa na Umoja wa Mataifa
kupeleka salamu vijijini ili kukabiliana na tatizo la mazingira na
mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanafumua misimu ya kilimo na
upatikanaji wa mvua. Kushirikisha vijana ni suala la msingi sana, hasa
ikizingatiwa kwamba sehemu kubwa ya vijana wanatoka vijijini ambako
malengo ya maendeleo endelevu yana maana zaidi kwa umma, alisema Kidai
Kabula Shaban, Mwanafunzi anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na
Kazi za Jamii.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel
Mosses akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez kuendesha semina ya malengo ya dunia
(Global Goals) kwa wanafunzi wa chuo hicho iliyofadhiliwa na Umoja wa
Ulaya (EU).
Amesema
amefurahishwa mno na mpango huo wa kuelimisha vijana hasa utunzaji wa
mazingira ili kukabiliana na tabia nchi. Alisema yeye alivyoelimishwa
basi atahakikisha anawaelimisha wengine kuwa watekelezaji wa maendeleo
hayo. Akirejea mazungumzo ya mwanafunzi huyo kwa niaba ya wenzake.
Alvaro alisema amefurahishwa na mwamko wa vijana wa kutaka kujua malengo
hayo na ni imani yake kwamba kwa kuwakujua wao basi jamii itaerevuka
mapema zaidi.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina kuhusu malengo
ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo
Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mtaalam
wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu
akiwapiga msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya
wakati wa semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mtaalam
wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu
akifafanua jambo wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu
(SDGs) kwa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya iliyofadhiliwa na
Umoja wa Ulaya (EU).
Mwalimu
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini Mbeya, Furaha Komoro
akiuliza swali kuhusu juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha
usawa wa kijinsia unakuwa na uwiano sawa pande zote.
Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji akishiriki kutoa maoni kwenye semina
ya malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa na kufadhiliwa na
Umoja wa Ulaya (EU).
Mwanafunzi
anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na Kazi za Jamii chuoni hapo,
Kidai Kabula Shaban akiuliza swali kwa mkufunzi (hayupo pichani) wa
malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Pichani
juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji
jijini Mbeya walioshiriki semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mmoja
wa washiriki akipitia kijarida cha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
katika semina iliyofanyika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya.
Picha
juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika
picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha
jijini Mbeya waliohudhuria semina ya malengo ya dunia (Global Goals)
iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Pichani
juu na chini ni semina maalum ya mabalozi wa malengo ya maendeleo
endelevu (SDGs Champions/Global Goals Champions) wakipigwa msasa wa SDGs
na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce
Temu (hayupo pichani).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi cheti kwa Balozi wa
Malengo ya Maendeleo Endelevu (Global Goals Champion) Manafunzi wa Chuo
Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) ambaye pia ni mrembo wa taji la Miss
Mbeya 2016, Eunice Robert.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi
wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wakiwa
wameshikilia vyeti vyao mara baada ya kuhitimisha semina maalum kwa
mabalozi hao.
No comments:
Post a Comment